March 7, 2017

UWT MKOA WA IRINGA WAWAKUMBUKA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA, WAFANYA USAFI SOKO KUU NA RC MASENZA PAMOJA NA DC KILOLO, IRINGA NA MBUNGE KABATI

mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wa pili kutoka kulia akifanya usafi soko kuu la Manispaa ya Iringa na umoja wa wanawake wa CCM Manispaa ya Iringa katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani itajayofanyika kesho machi 8,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah, Kulia kwake ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na katibu wa UWT mkoa wa Iringa na wanachama wengine
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akifanya usafi leo
UMOJA wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT)  mkoa wa Iringa umefanya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kuwatembelea vijana walioathirika na dawa za kulevya waliopo kituo cha Iringa Sober House kutoa msaada. 
Akiwashukuru UWT mkoa wa Iringa mara baada ya kushiriki kufanya usafi soko kuu la Manispaa ya Iringa leo kabla ya kwenda kutoa msaada huo, mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema Wanawake hao wameonyesha mfano mwema kwa jamii 
Kuwa kuwasaidia vijana hao walioathirika kwa matumizi ya dawa za kulevya ni jambo la msingi na kuwataka wanawake kuwa mbele kupiga vita vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE