March 3, 2017

UTUMISHI YAKABIDHIWA MAGARI MAWILI NA JICA

MAG1
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) akimwakilisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA), Bw. Toshio Nagase (kulia) katika hafla fupi ya kupokea magari mawili (2) yaliyotolewa na JICA leo katika ukumbi wa JICA.  
MAG2
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA, Bw. Toshio Nagase (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari kwa Ofisi ya Rais -Utumishi katika ukumbi wa JICA mapema leo. Wa kwanza kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Mahusiano kwa Umma wa JICA, Bw. Raymond Msoffe.
MAG3
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi wa Ofisi ya Rais–Utumishi, Bw. Peter Mabale akihakiki vibali vya mojawapo ya gari lililokabidhiwa kwa Ofisi ya Rais – Utumishi kutoka JICA.
MAG4
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (katikati) akipokea funguo za magari kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi Dr. Laurean Ndumbaro kutoka kwa  Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase (kushoto) katika ofisi za JICA mapema leo.
MAG5
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Rais- Utumishi na JICA mara baada ya hafla ya makabidhiano ya magari katika ofisi za JICA jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………….
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo imekabidhiwa   magari mawili kutoka Shirika la Kimataifa la  Maendeleo la Japan (JICA)  kwa matumizi ya ofisi.
Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa JICA Bw. Toshio Nagase akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema  JICA imekabidhi magari hayo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na JICA.
JICA imetoa msaada wa magari kwa Ofisi ya Rais-Utumishi ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya ofisi hizo mbili.
Wakati wa hafla hiyo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu-Utumishi Bw. Mick Kiliba alisema Tanzania imekuwa kati ya nchi zinazonufaika na misaada kutoka nchini Japan.
“ Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo Elimu, Miundombinu, Afya, Maji na Maendeleo ya rasilimaliwatu na leo ninafuraha kuona ushirikiano huu unaendeleza urafiki wetu” Bw. Kiliba alifafanua.
Bw. Kiliba aliishukuru JICA na Serikali ya Japani kwa msaada wa magari hayo.
“Kwetu sisi ni msaada mkubwa sana. Magari haya yataleta mabadiliko chanya kwa kuongeza uwajibikaji na utoaji huduma bora kwa umma”
Bw.Kiliba aliahidi kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI itahakikisha inayatunza na kuhakikisha yanafanikisha lengo la Ofisi la kutoa huduma bora.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE