March 11, 2017

USAFI IRINGA KILA JUMAMOSI ATAKAEPUUZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI -RC MASENZA


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akifanya usafi nje ya soko kuu la Manispaa ya Iringa na wanawake wa UWT Irina, kulia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati
..........................................................................
Na Matukiodaima blog

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ameagiza wananchi wa mkoa wa Iringa kufanya usafi kila jumamosi katika maeneo yao na atakaye kaidi kufikishwa mahakamani.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo leo kuwa amejifunza na kupendezwa na utamaduni wa wakazi wa Dar es Salaam ambao kila jumamosi kwao ni siku ya usafi na kuwa Kwa utamaduni huo utasaidia kuweka mkoa wa Iringa katika hali ya usafi .

Hivyo alisema katika mkoa wa Iringa maeneo yote ya biashara kabla ya kufunguliwa watawajibika kuanza Kwa usafi na siku za jumamosi biashara zote zitafunguliwa kuanzia saa tatu asubuhi.

"Ninaagiza kuanzia jumamosi ijayo kila mfanyabiashara kabla ya kufungua biashara yake kufanya usafi eneo lake na maeneo yote ya biashara muda wa kufungua ni saa tatu asubuhi atakaye fungua mapema atakamatwa na kufikishwa mahakamani"

Hivyo aliwataka viongozi wote wa mitaa hadi wilaya kusimamia agizo hilo na kutosita kuchukua hatua kwa wote watakaopuuza agizo hilo.

Masenza alisema mkoa wa Iringa ni mmoja kati ya mikoa ambayo imekuwa ikifanya vema katika usafi hivyo hata kubali kuona uchafu unachukua nafasi katika mkoa huo.

Alisema jumamosi tatu kwa mwezi ni zamu ya wafanyabiashara kufanya usafi maeneo yao na jumamosi ya mwisho wa mwezi ni zamu ya wananchi wote kufanya usafi kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Magufuli.

Pamoja na kufanya usafi bado alisema kila jumamosi wananchi wote wa mkoa wa Iringa watalazimika kutekeleza agizo la makamu wa rais la kufanya mazoezi ya pamoja katika uwanja wa Samora

Masenza alisema maagizo yote hayo ya serikali yamelenga kuboresha afya za wananchi wa Tanzania hivyo utekelezaji wake ni wa lazima kufanywa na kila mmoja na Iringa hatakubali kuona mtu anapuuza agizo hilo.

Mwisho

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE