March 26, 2017

UNYAMA :WANAMGAMBO 40 WACHINJWA DRC


Polisi wa kupambana na ghasia wa DRC wakiondowa vizuizi vya barabarani Kinshasa December 10, 2011.

Polisi wa kupambana na ghasia wa DRC wakiondowa vizuizi vya barabarani Kinshasa December 10, 2011.

Karibu maafisa 40 wa polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameuliwa kwa kukatwa katwa na wanamgambo wa kundi la Kamwina Nsapu katika jimbo la kati la Kasai.
.................................................
Karibu maafisa 40 wa polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameuliwa kwa kukatwa katwa na wanamgambo wa kundi la Kamwina Nsapu katika jimbo la kati la Kasai.

Kufuatana na rais wa bunge la Kasai Francois Kalamba, wanamgambo hao walishambulia msafara wa magari ya polisi waliokua wanasafiri kutoka mji wa Tshikapa kuelekea mji mkuu wa jimbo la Kasai wa Kananga waliposhambuliwa Ijuma na wanamgambo hao.

Kalamba anasema mashahidi wameeleza kwamba wanamgambo waliwaachilia huru maafisa sita kwa vile walikua wanazungumza lugha ya Tshiluba inayotumika eneo hilo.

Anasema wanamgambo hao ambao kawaida huwa na mapanga, waliiba bunduki na silaha za polisi na kukimbia pamoja na magari yao.

Uwasi katika eneo la kati ya DRC ulianza mwezi Ogusti mwaka jana na umeenea katika majimbo kadhaa ya eneo hilo.

Hata hivyo siku ya Jumamosi wizara ya mambo ya ndani ya serikali kuu imetangaza kwamba kuna wanamgambo 400 wamejisalimisha wiki hii katika jimbo hilo la Kasai.#chanzo VOA #

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE