March 9, 2017

TUKIO LA KINYAMA UJUMBE TOKA MITANDAO YA KIJAMII LEO

TAARIFA YA TUKIO KWA KIREFU

KOSA : MAUAJI

MNAMO TAREHE 07/03/2017 SAA 17.00HRS MTOA TAARIFA (KE), CHAGA, 30YRS, KIBAMBA  24YRS,  ANAELEZA KUWA MAJIRA YA SAA 10.00HRS HUKO KIBAMBA ALITUMIWA MESEJI KWENYE SIMU YAKE ILIYOSEMA
'' NENDENI MKACHUKUE MAITI YA NDUGU YENU ITAOZEA NDANI'' KUPITIA NAMBA YA SIMU YA DADA  YAKE AMBAYE NI MAREHEMU (KE), DIGO, 34YRS , MAMA WA NYUMBANI, MKAZI WA KIBAMBA!
BAADA YA KUPATA UJUMBE HUO ALIOGOPA NA KUANZA KUWATAFUTA NDUGU ZAKE WENGINE NA NDIPO MAJIRA HAYO ALIAMUA KWENDA KITUO CHA POLISI KUTOA TAARIFA AMBAPO  BAADA YA TAARIFA KUPOKELEWA,ALIONGOZANA NA ASKARI MPAKA NYUMBANI KWA MAREHEMU NA KUKUTA, GARI YAKE NO T 827 CYS AINA YA NISSAN MOCO IKIWA NJE YA UZIO WA NYUMBA YAO AMBAPO INASEMEKANA ILIKUWEPO ENEO HILO TOKEA TAREHE 2/03/2017, BAADA YA KUINGIA NA KUVUNJA MLANGO WA  CHUMBA CHA KULALA ULIKUTWA MWILI WA MAREHEMU UKIWA UMEHARIBIKA NA KUWEKWA NDANI YA JABA LA MAJI!

 UCHUNGUZI WA AWALI
 ENEO LA TUKIO UNAONYESHA KUWA MAREHEMU AMEUAWA AIDHA NA MUME WAKE AITWAYE (ME) NYAMWEZI, UMRI HAUFAHAMIKI, JWTZ KAMBI YAKE BADO KUFAHAMIKA AMBAYE KWA SASA INASEMEKANA YUKO ZANZIBAR KWA MAFUNZO NA KUNA MASHAKA MAKUBWA YA KUHUSIKA NA MAUAJI HAYO KWANI ENEO LA TUKIO VIMEKUTWA VIPIMO VYA HIV VIKIWA VIMETUMIKA AMBAVYO ALIPENDA KUVITUMIA KWA KUPIMA AFYA YAKE NA INAAMINIKA KUWA HUENDA BAADA YA KUBAINI KUWA KUNA TATIZO HILO NDIPO ALIFANYA MAAMUZI HAYO! AIDHA HATA KWENYE SIMU YAKE HAPATIKANI. UCHUNGUZI UNAFANYWA KUJUA ALIPO MUME WA MAREHEMU ILI AWEZE KUHOJIWA KUHUSU TUHUMA HIZO.
MWILI UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI.
TUKIO LIMEKAGULIWA NA OC CID KIMARA ASP BONIFACE, INSP GLORY NA KUNDI LA MAKACHERO.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE