March 10, 2017

TUIANZE SIKU HII YA IJUMAA KWA KUMSHUKURU MUNGU....
 Mwenyenzi Mungu mwingi wa Rehema tunakushukuru ahsante Kwa kuwa nasi usiku kutwa ni mengi mabaya dhidi yetu umetuepusha 

Nasi hatuchoki kukutukuza wewe maana sisi ni wahitaji siku zote 

Katika zaburi 14:1-3
 Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu wameharibu matendo yao na kufanya chukizo hakuna atendae mema 

Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu aone kama yupo mtu mwenye akili amtafutaye Mungu ,wote wamepotoka wameoza pamoja hakuna atendaye mema la !hata mmoja 

Bwana si hivyo twatambua si Kwa uwezo wetu ni kwa uwezo wako tupo hai na tupo kukuomba hekima yako asubuhi hii tembea nasi Kazini, safarini, na hata mahospitalini ukawaponye wagonjwa, tumepoteza wapendwa wetu siku hii ya leo Mungu tufute machozi ukatunyamazishe maana sote tuwasafiri.

Tunaendelea Mungu kukushukuru kwa mvua na tunaomba uzidi kutushushia Mvua ili mazao yetu mwaka huu tupate zaidi japo tunaomba mvua ya kiasi yenye kuleta neema na sio mvua yenye maafa ya mafuriko, kipundupindu au kuleta vifo 

Tusikie Mungu katika maombi yetu tubariki sote na familia zetu zote 

Naomba wote kwa kumueshimu Mungu na ukiona ni vema kumshukuru Mungu inakupasa na unatamani kuona mema hapa duniani sema 

AMEN..... 

nikutakie siku njema yenye baraka

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE