March 5, 2017

TRUMP ATOA AGIZO LA KUCHUNGUZWA KWA OBAMA JUU YA MATUMIZI MABAYA YA IKULU

Donald Trump


Rais wa Marekani Donald Trump ametaka bunge la Congress kuchunguza ikiwa Barack Obama alitumia vibaya mamlaka yake wakati wa kampeni ya uchaguzi siku moja baada ya kudai kuwa Obama alikuwa akidukua simu zake.
Msemaji wa Trump alisema kwa uchunguzi kuhusu kuingia kwa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekanai utasaidia uchunguzi huo.
Trump alitoa madai hayo kwenye mtandao wa tittwer lakini hakutoa ushahidi wowote.
Aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Marekani James Clapper, wakati wa kampeni alikana kuwa mawasiliano kwenye jumba la Trump Tower hayakunakiliwa.
Msemaji wa Obama Kevin Lewis, alisema kuwa rais huyo wa zamani hakuwai amrisha kudukuliwa kwa raia yeyote wa Marekani.
Trump ambaye anakabiliana na uchunguzi mkubwa unaohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani, alitoa madai hayo kupitia mtandoa wa titter akiwa jimbo la la Florida siku ya Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE