March 18, 2017

TAZAMA PICHA ZA MAZOEZI BAADA YA RC IRINGA KUNUSURIKA AJALI LEO MARCH 18/2017, MWENYEKITI WA CCM ALIYETUMBULIWA AWA KIVUTIO

Mwenyekiti  wa CCM Iringa  mjini Abed  Kiponza (mwenye sare za CCM ) ambae  alivuliwa nafasi yake na kupewa  onyo kali na CCM baada ya  kudaiwa  kusaliti  chama  wakati wa kampeni awa  kivutio mazoezi ya  viungo  uwanja wa Samora  mkoani Iringa leo hii ni jumamosi ya  kwanza  kujumuika mazoezi  toka  alipotumbuliwa 
viongozi  mbali mbali  wa  wilaya ya mkoa  wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wa pili  kulia  wakiwa katika mazoezi  wa kwanza  kulia ni mkuu wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  na wa tano ni katibu tawala  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayubu 
kiponza  akifanya  mazoezi  kimadoido 
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza wa pili  kulia akifanya mazoezi  ya  viungo uwanja wa Samora  leo 

Wamoja  Ayubu  akiwajibika kimazoezi 
Kiponza  akipiga  picha za  kumbukumbu na  wadau wa usalama barabarani  mkoa wa Iringa 
Bado  naipenda  CCM asema  kiponza 
Kiponza  akiwaeleza jambo  viongozi wa mkoa wa Iringa wakati  wakitoka katika mazoezi 
Usalama  wa  kutosha mazoezi ya  viungo  mkoa wa Iringa 
Askari  wa  usalama  barabarani  akiongoza mazoezi 
Kiponza  akiwavunja mbavu  viongozi  juu ya  kutemwa kwake  uenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini


Kumbuka jumamosi  ijayo  hakutakuwa na mazoezi ya  viungo  mkoa wa Iringa badala yake  wananchi  wote  wa mkoa wa Iringa  watashiriki siku ya usafi ya  kitaifa  na  serikali ya  mkoa wa Iringa  imeagiza  jeshi la polisi  kuwakamata wote  watakaofungua  biashara  zao kabla ya saa 3 asubuhi  wakati  mkuu wa mkoa atafanya ukaguzi  nyumba kwa  nyumba kwa  wale  watakaokutwa wachafu  kuwajibika .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE