March 28, 2017

TAIFA STARS YAIGAGADUA BURUNDI 2-1

SAFARI ni safari hii leo timu ya Taifa la Tanzania Taifa Stars imeweza kuonyesha ni Safari yenye mafanikio katika michezo ya kirafiki baada ya kuigagadua Burundi 2-1 katika mwendelezo wa mechi za kirafiki chini  ya kocha Mzalendo Jackson Mayanja .

Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ulichezwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam ambapo ni wa pili kwa kikosi kipya cha timu ya Taifa chini ya Mayanja.

Kinara wa kupachika mabao katika ligi kuu Tanzania bara Simon Msuva alitangulia kuipatia Taifa Stars bao la kwanza bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Burundi walizinduka na kusawazisha bao hilo likifungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo anayeichezea Simba SC Laudit Mavugo baada ya mabeki kuchanganyana na mkali huyo wa kupachika mabao kufunga kirahisi.

Mshambuliaji mpya wa Taifa Stars Mbaraka Yusuph ambaye huichezea pia Kagera Sugar ya mkoani Kagera ndiye aliyerudisha tabasamu katika nyuso za Watanzania akifunga bao la ushindi kwa Taifa Stars zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mpira kuisha.

Taifa Stars leo ilicheza bila ya nahodha wake Mbwana Samata ambaye ameshaondoka nchini kurudi Ubelgiji kwaajili ya mechi ya ligi ya huko wikiend hii akiwa na klabu yake ya Genk.

Ushindi huu umekuja siku chache baada ya kuwafunga Botswana katika mechi iliyochezwa Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE