March 28, 2017

TAASISI YA DBL YAWAKUTANISHA WANAWAKE VIONGOZI MKOA WA IRINGA NA MBEYA

Baadhi ya wanawake viongozi wa dini na wa jamii wakiwa katika warsha ya wanawake
Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa John Kiteve akipokea zawadi Kwa ajili ya mkuu wa mkoa Iringa

........................................

TAASISI inayojihusisha na huduma za kiroho na malezi ya watoto yatima mkoani Iringa ya Dairy Bread Life(DBL) imewakutanisha wanawake viongozi wa dini na viongozi wa kijamii mkoa wa Iringa na Mbeya kwa lengo la kupeana mbinu na maarifa ya kuitumikia jamii na kukemea matukio yaubakaji na ulawiti.

  Mraribu wakongamono hilo Mchungaji Neema Mwaisumbe alisema hayo jana mjini Iringa kuwa wamelazimika kukutanakatika kongamano hilo ili kuweza kuikomboa jamii kupitia wanawake hao ambao niviongozi na wake wa viongozi. 

 Hivyoalisema kuwa njia pekee ya kuweza kuondokana na maasi katika jamii ni wanawakehao kusimama pamoja kuikomboa jamii Kwa kueneza elimu hiyo.

  Alisema kupitia kongamano hilo wanawake wataifanya kazi maalum ya kuikomboa jamii ya kitanzania kwa kuifanya kwa ufanisi zaidi ili kupitia wanawake hao viongozi wanawakewengine wakabadilika kwa kuelekeza nguvu zao katika maeneo mbalimbali. 

“Wanawake tunayonafasi kubwa sana ya kuelimisha umma mzima kuhusu kuigeuza jamii kuepukana na maasi mbali mbali yanayoendelea na kulifanya Taifa kuwa salama pasipo vitendo viovu “ 

Aidha alisema kuwa sababu kubwa ya watu kuwaonea huruma watuhumiwa wa makosa ya ubakaji ni kutokana na kutokuwa na elimu hivyo iwapo jamii nzima itaelimika hakutakuwa na mtu anayetetea wabakaji zaidi ya kuwafichua . 

Mgenirasmi katika kongamano hilo mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenzaaliyewakilishwa nafisa ushirika mkoa wa Iringa John Kiteve aliwataka wanawakehao kujitambua na kuangalia ni namna gani roho zao ni safi na zipo kwa ajili yakukomboa jamii.  

Kwanialisema hata maandiko yanasema roho idumuyo ni ile yenye mahusiano mazuri naMungu hivyo lazima kufanya mema kwa kumkaribisha Yesu Kristo ili kuitegemeaTaifa. 

 "Hakunamtu ambae ameumbwa kwa bahati mbaya ila wote tumeumbwa kwa mapenzi na makusudiya Mungu.... Wapo wengine ambao wanajidharau wenyewe " 

Aliwatakawanawake wao na jamii kwa ujumla mara zote kuwa kama vile ulivyo na siovinginevyo. 

 Mkuu huyowa mkoa alipongeza hatua ya kuandaa kwa kusanyiko hilo kwani anaamini ni ukombozina suluhisho la jamii kwa mkoa wa Iringa. 

 Mkurugenzi wa taasisi ya Dairy Bread Life(DBL) mchungaji Mpeli Mwaisumbe ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo alisema kuwa wamekuwa na kawaida ya kila mwaka kuandaa kongamano kama hilo nakuwa kongamano lijalo litahusu wanaume viongozi na wasio viongozi na linatagemewa kufanyika mkoani Mbeya huku akishukuru wadau wakubwa wa kufanikisha suala hilo

Askofu Floyd Parker na mkewe Bonnie kutoka jimbo la Teleios nchini Marekani 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE