March 17, 2017

SIR GEORGE KAHAMA NA SAFARI YAKE YA MWISHO DUNIANI

1
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa  salamu za pole kutoka Serikalini katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama  aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo  limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
2
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw.Abdurahaman Kinana akitoa salamu za rambirambi za Chama wakati wa  kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo  limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
3
Jaji Mstaafu Mhe.Joseph Sinde Warioba akitoa salamu za pole wakati wa  kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama  aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo  limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere  Dar es Salaam.
4
Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa  salamu za pole katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  tukio  hilo  limefanyika leo  katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
5
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa  heshima za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,  tukio hilo  limefanyika leo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
6
Rais wa awamu ya pili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa  heshima za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio  hilo  limefanyika leo  katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
7
Makamu wa Rais mstaafu  katika Serikali ya awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akitoa  heshima za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio  hilo  limefanyika leo  katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
8
Mjane wa Marehemu Sir. George Clement Kahama Mama Janet Kahamawa (pili kushoto) akiwa na familia yake wakati wa Tukio la kumuaga mume wake ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania  katika nyadhifa mbalimbali  aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio  hilo  limefanyika leo  katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Serikali imesema itaendelea kuenzi na kuheshimu mchango mkubwa katika kupigania maendeleo na ustawi  wa jamii uliofanywa na  marehemu Sir George Kahama  enzi za uhai wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akitoa salamu za Serikali katika tukio la kumuaga mmoja wa waasisi wa Taifa na Waziri msataafu marehemu Sir Gorge Kahama aliyefariki dunia Machi 12 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waziri Nape amesema kuwa Sir George Kahama alikuwa kiongozi mahiri na aliyetekeleza majukumu yake kwa ufasaha ambapo alikuwa miongoni mwa viongozi walioanzisha harakati za Serikali za uendelezaji  wa mji wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya  kuimarisha makao makuu ya nchi.
“Marehemu Sir George Kahama tutamuenzi kwa kuendeleza yale mazuri aliyoyafanya katika kuijenga nchi yetu hasa katika ustawi wa jamii na kuimarisha uchumi wa nchi”.Alisema Waziri Nape.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Abdurahaman Kinana amumueleza Sir George Kahama kama kiongozi mahiri katika Chama aliyependa maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla katika weledi wa hali ya juu na alikuwa mchapakazi.
“Sir George Kahama alikuwa mtumishi na kiongozi aliyetukuka  ametuachia hamasa kubwa ya kuwa viongozi bora zaidi na wenye mapenzi na Taifa letu katika kuleta maendeleo.”Alisema Ndugu Kinana.
Marehemu Sir  George Kahama amekuwa Waziri na Kiongozi kabla na Baada ya Uhuru wa Tanzania  Bara kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amezikwa leo Jijini Dar es Salaam na ameacha Mjane na Watoto.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE