March 8, 2017

SIKU YA WANAWAKE, TUIANZE KWA SALA

LEO NI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HONGERA MAMA:

Mali akili na vyote ni mali ya Mungu na wewe si wa kwanza kuwa na mali ama akili hapa duniani wapo wengi leo wamekufa hivyo usijikweze...

Tuinze siku hii ya wanawake duniani kwa kumtanguliza Mungu pia kumshukuru kwa kuwalinda mama zetu na sisi sote jiulize bila mama leo wewe ungekuwa wapi? Ahsante Mungu kwa kumlinda mama ahsante kwa kuendelea kuwapigania wanawake wote

Mungu tumeshuhudia baadhi ya wanaume wakiwatukana wake zao ama wanawake wengine kwa kuwaita golikipa eti kama tusi kwao ila ukweli ili timu iweze kushinda ni lazima kipa awe bora mdakaji mzuri ndio maana timu bora duniani ni zile zenye kipa bora na beki mpira ukimshinda hurudisha kwa kipa kwa ajili ya kupanga mashambulizi upya hivyo leo napenda kuwapongeza wanaume wote wanaoita wanawake goli kipa maana mwanamke ni msimamizi wa familia si vibaya ukipata pesa za mshahara kurudisha nyumbani kwa mwanamke ili apange matumizi

Ahsante Mungu kwa kuwalinda wanawake wote tunaomba waepushe na vitendo vya ukatili dhidi yao kama ubakaji na vingine

Asubuhi hii wapo wanawake wanaoteseka kwa kukosa Masada wa matibabu ama kutelekezwa au ajira Mungu uwe katikati yao wape msaada

Wabariki wote wanaosafiri maeneo mbali mbali leo mpe afya njema makamu wa Rais mama Samia na viongozi wote wanawake

Tunasema ahsante kwa Tanzania yenye amani ahsante kazi nzuri ya Rais wetu tunaomba umlinde na mabaya

Kipekee Mungu tunaonba ulinzi wako wadau wa matukiodaimablog wote na familia zetu

Amen

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE