March 13, 2017

SI KILA MAZIWA NI BORA KWA AFYA YAKO TUMIA MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD


        MARA nyingi watu wengi wamezoea kula au kunywa kile kinachopatikana na si kile kinachotakiwa(kinachohitajiwa). Tabia hii huchangiwa na mambo mengi kama ukosefu wa fedha, muda wa maandalizi, mila na desturi

        pamoja na sababu hizo, moja kubwa linalochangia ni ukosefu wa elimu sahihi ya vyakula. Bila ya kujua faida ya kitu unachofanya au unachotaka kufanya hakika hautatilia mkazo. Baada ya kuona aina za maziwa huko nyuma, leo tuyaangalie faida zake katika miili yetu.

        MAZIWA kama yalivyo hayawezi kutengenezwa kiwandani. Ni lazima yatokane na wanyama hasa wanyama wanyonyeshao (Mamals). Na hayapatikani pasina wanyama kuzaa, hivyo kuhitajika kumnyonyesha mwana. Na sehemu katika lishe ya mwanae

        ndio sisi huitumia. Na kwa minajili hiyo, basi maziwa ni lishe tosha. Ndugu msomaji hata kabla ya kueleza faida tuzipatazo kutokana na maziwa, hebu tumfikirie mtoto mchanga. Mtoto aliyezaliwa leo anaishi kwa kunyonya tu takriban miezi minne au sita. Bila

        mjadala ni kwamba maziwa yamebeba mahitajio yote muhimu katika kujenga mwili, kuupa mwili nguvu na joto na kuulinda mwili na magonjwa.

        Maziwa hutupatia takriban vitamini zote ambazo huyeyuka kwenye mafuta. Nazo ni vitamini A, D, E na K. Vitamini A huhusika na shughuli mbalimbali mwilini. Mfano afya bora ya ngozi zetu kuwa nyororo na ng'avu na pia kuwa na uwezo wa kuzuia wadudu

        wasiingie mwilini. Vile vile vitamini A hutumika pia kuyapatia macho uimara wa kuona. Na hasa kuona usiku au kwenye mwanga hafifu. Ukosefu wake hudhoofisha macho na hata kuleta upofu, ngozi kusinyaa na kuonekana iliyozeeka hata kama ni ya kijana.

        Vitamini D husaidia mwili kuweza kufyonza madini ya kalsiamu. Bila kuwepo vitamni D kalsium hupotea bure kwa kutolewa nje kama kitu kichohitajika. Japokuwa vitamini D tunaweza kuipata kwenye jua la asubuhi, watu wengi hawawezi kulipata jua hilo.

        Labda kwa kuishi magorofani au chini ya milima au kutoweza kutoka nje nyakati za asubuhi. Hivyo ni bora kujiwekea uhakika wa kupata vitamini D kwa kunywa maziwa.

        Umuhimu wa madini ya Calcium ni kiungo muhimu katika ujengaji wa mifupa. Hasa kwa wajawazito na watoto ambao mifupa yao bado inajengeka. Mwili imara hubebwa na mifupa imara. Na mifupa imara inajengwa na madini ya Kalsium. Ni bora kujijengea

        mifupa imara, meno na sehemu ya mifupa. Hakika kila mtu anahitaji meno bora na imara, vile vile kalsium hutumika katika misuli (muscle) wakati wa kujikunja na kunyooka. Pia husaidia katika mtandao wa ufahamu mwilini (nerve conduction). Kwa ufupi hayo ni manufaa ya kunywa maziwa, samaki na kadhalika. Mbali na Kalsium maziwa hutupatia madini ya salfa, sodium na phosphoras ambayo mwili pia huhitaji kwa kazi zake mbalimbali.

        Maziwa pia hutupatia protini kwa ujengaji wa miili yetu. Mathalan mtoto mdogo wa siku moja huongeza ukubwa na uzito kwa kunywa au kunyonya maziwa tu. Japokuwa kiwango cha protini hutofautiana kulingana na mnyama, pia maziwa ya ng'ombe yana protini ya kutosha. Hali kadhalika katika maziwa ya mbuzi na kadhalika.

        Maziwa pia hutupatia sukari (wanga) japo kwa kiasi kidogo lakini kidogo chafaa kuliko kukosa. Na ndio maana japo kwa kunywa maziwa waweza kuhisi nguvu iwapo ulikuwa na njaa.

        Nyakati za baridi, maziwa hutumika kama kinywaji moto. Yenyewe peke yake kwenye chai, kahawa au tangawizi. Na wakati wa joto, maziwa hutumika kama kipozeo na kiburudisho tosha. Na kwa nyakati hizi, kila sehemu inaweza kupatikana na maziwa. Kwa asiyependa tunamshauri aanze kuyapenda na kuyatumia.

        Maziwa pia hutumika kama dawa kwa kuchanganywa na vitu mbalimbali. Mathalani maziwa ya mama yakamuliwapo kwenye jicho linalowasha, uchafu hotoka na kujihisi salama.

        Kwa kuzingatia umuhimu wa maziwa kama tulivyoona kwa ufupi, kwa kauli moja tunaisisitiza jamii kunywa maziwa katika milo ya kila siku. Na vile vile kama kiburudisho wakati wowote. Ni hasara kupoteza fedha zako kununua vinywaji visivyo na faida kubwa

        kama tuipatavyo katika maziwa, mathalan soda, na juice za makopo ambazo zimejaa rangi, maji na sukari na madawa bila ya virutubisho vyovyote vingine. Tumia pesa zako kwa malengo maalum. Jenga afya yako, kunywa maziwa.

Na si kila maziwa ni bora kwa afya yako ugopa maziwa yasiyo na ubora yapo maziwa yanayouzwa mitaani ambayo si maziwa ni rangi ya maziwa wanachanganya maziwa maji

Kipekee nipongeze maziwa ya Asas Dairies ltd kutoka mkoani Iringa kwa kuendelea kushika soko la ubora wa maziwa kwa miaka zaidi ya minne sasa


Hivyo huna sababu ya kununua bora maziwa tumia maziwa ya Asas Dairies Ltd yanayopatikana nchi nzima

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE