March 2, 2017

SERIKALI KUWAFIKIA WATOTO WOTE WA KIKE NCHINI


1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea katika ufunguzi wa majadala kuhusu ukatili wa kijinsia dhidi ya waanawake na wasichana unavyokuwa kikwazo cha ukombozi wa wanawake kiuchumi katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani leo jijini Dar es Salaam.
2
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  ufunguzi wa majadala kuhusu ukatili wa kijinsia dhidi ya waanawake na wasichana unavyokuwa kikwazo cha ukombozi wa wanawake kiuchumi katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani leo jijini Dar es Salaam.
Na Anthony Ishengoma- MOHCDGEC
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali inakusudia kuanzisha kampeni ya kitaifa kumfikia mtoto wa kike popote Nchini ili aweze kujitambua yeye ni nani ikiwemo umuhimu wa kujitambua kiafya na kujijengea ufahamu wa kujiendeleza kitaaluma kwani ndiyo nguzo muhimu ya kujiletea maendeleo ya  kiuchumi.
Waziri Ummy Mwalimu mesema hayo wakati akifungua mjadala kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unavyokuwa kikwazo cha ukombozi wa wanawake kiuchumi katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Mjadala huo unaendelea  katika ukumbi wa mikutano wa shirika la Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) na  kilele cha maadhimisho hayo ni Machi 8, mwaka huu.
Aidha aliwaambia washiriki wa mkutano huo kuwa serikali haina tatizo katika kutunga sera na sheria zinazolenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana  bali kuna baadhi ya changamoto zinazoitaji msukumo ambazo ameziita za kiutekelezaji akisema kila awamu ya serikali imekuwa ikifanyia masuala mbalimbali yanayohusiana na sheria na sera hizo.
Waziri Mwalimu aliendelea kusema kuwa kwa kuzingatia hilo, serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutunga sera, sheria na miongozo mbalimbali, pamoja na kuweka mipango na mikakati ya Kitaifa na Kisekta ili kuhakikisha kuwa wanawake wanapatiwa fursa mbalimbali za kuwawezesha kiuchumi.
Waziri alongeza kuwa katika kuwezesha wanawake kiuchumi pia Serikali imeanzisha Benki ya Wanawake, mifuko mbalimbali ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na Majukwaa ya kuwezesha Wanawake Kiuchumi, ili kuwawezesha wanawake kupata mikopo yenye masharti nafuu.
Akifafanua kuhusu mfuko wa maendeleo ya wanawake Waziri amesema Wizara imeendelea kuhamasisha Halmashauri kuchangia asilimia tano  (5%) ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ambapo kwa kipindi cha Mwezi Julai,  hadi Disemba, 2016 kiasi cha Shs 6,222,164,982 zilitolewa na Halmashauri 101 kwa ajili ya kuwakopesha wa wanawake wajasiriamali. 
Aidha aliongeza kuwa idadi ya Wanawake wanaoshiriki katika mifumo rasmi ya kifedha imeendelea kuongezeka ingawa kiwango chao cha ushiriki bado ni cha chini ikilinganishwa na wanaume.
Aidha aluambia mkutano huo kuwa wanawake wanaotumia huduma  rasmi za kifedha  waliongezeka kutoka asilimia ya 44.5 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 84 mwaka 2016 ikilinganishwa na wanaume waliongezeka kutoka asilimia 44.4 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 88 mwaka 2016.
Aliendelea kusema kuwa dhamira ya serikali  ni kuhakikisha kuwa uwezeshwaji huu unawafikia wanawake wengi zaidi hususan wanaoishi pembezoni huku akibainisha kwamba ni dhahiri kuwa uchumi kwa mwanamke unaleta mabadiliko ya haraka ndani ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Akiongelea fursa za kisiasa na nafasi za juu katika ajira Waziri amesema anatambua bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia usawa 50/50. Kwasasa tumeweza kuweka usawa kikatiba kwa kuwa na asilimia 36 ya uwakilishi wa wanawake bungeni. Pia, usawa katika usaili wa wanafunzi katika shule za msingi, hata hivyo, bado changamoto zipo katika utendaji na nguzo za kimahakama, pamoja na kupata nafasi za juu serikalini.
Naye Barozi wa Sweden hapa Nchini Tanzania Katrina Rangnitt aliwaambia awajumbe wa mkutano huo kuwa ni muhimu jamii ya Tanzania ikaachana na mila potofu zinazoendelea kumkandamiza mwanamke na kutaka kuwepoa kwa usawa wa kijinsia unaomfanya mwanamke kuwa huru kimaamzi.
Aliongeza kuwa ana taarifa kuwa Tanzania ina sera shirikishi za ajira na wigo wa elimu umetanuliwa ili kuongeza nafasi za masomo kwa wanawake hapa nchini.
Katika juhudi kutokomeza ukatili wa kijinsia hapa chini Serikali tayari imezindua mpango mpango wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE