March 8, 2017

REA AWAMU YA TATU YAZINDULIWA RASMI KITAIFA MKOANI TANGA

1
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini  (Tanesco).Mradi huo umezinduliwa rasmi kitaifa katika kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga.
2
3
.Wakazi wa kijiji cha Zingibari Wilayani  Mkinga mkoani Tanga wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) wakati wa  uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Tanesco.
4
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani,(katikati), Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela( kushoto) na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhaga Mpina(kulia) wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga, Mawaziri hao walikuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi
5
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga alipofika kijijini hapo kuzindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme vijijini kitaifa unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini  (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Tanesco.
Na Zuena Msuya, Tanga
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme vijijiji ,unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu kitaifa kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco,utakao sambaza umeme kwa vijiji vyote ambavyo havikupata huduma hiyo wakati wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Zingibari  wilayani Mkinga mkoani Tanga, Dkt . Kalemani alisema kuwa, REA Awamu ya Tatu itatekelzwa kwa miaka mitano kuanzia sasa hadi kufikia 2021.
Dkt. Kalemani alifafanua kuwa,mara baada ya uzinduzi rasmi wa kitaifa wa mradi huo mkoani Tanga,Mikoa mingine itaendelea kuzindua mradi huo katika mikoa yao kulingana na makubaliano ya mikataba ya wakandarasi husika katika Mikoa hiyo.
“REA awamu ya Tatu imezinduliwa rasmi hapa mkoani Tanga, mradi huu sasa utamaliza kazi ya kuunganisha huduma ya umeme katika vijijini vyote 7867 nchini vilivyoachwa katika Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi huo, ili kifikia idadi ya vijiji vyote 12,262,Tanzania bara ifikapo  mwaka 2021”, alisema Kalemani.
Akizungumzia mradi huo kwa Mkoa wa Tanga, Dkt. Kalemani alisema kuwa REA Awamu ya Tatu itasambaza  huduma ya umeme katika vijiji 166,  ambapo  vijiji 20 kati ya hivyo ni vile ambavyo vilipitiwa na Mradi wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili lakini havikuunganishwa na huduma ya umeme , na vijiji 146 ambavyo havikupitiwa kabisa wala kuunganishwa na Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini iliyopita.
Aidha , Dkt. Kalemani alitoa wito kwa wakandarasi watakaotekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji wa huduma ya umeme nchini ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa nchi ya viwanda.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliwataka wakazi wa Mkoa huo waliokosa huduma hiyo katika miradi iliyotangulia, kutandaza nyaya za umeme katika nyumba zao ili kuweza kuunganishwa na huduma ya umeme  ambayo hupatikana kwa bei nafuu ya shilingi elfu 27 .
Aidha aliwataka wananchi hao kulinda na kuitunza miundombinu ya mradi huo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla kwa kuwa miundombinu hiyo ni ya gharama kubwa.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE