March 25, 2017

RC IRINGA APIGA MARUFUKU BIASHARA KUFUNGULIWA KABLA YA SAA 3 ASUBUHI JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI ......

Image result for RC Iringa

MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  ametaka  wananchi watakaofungua biashara  zao kabla ya  saa 3 asubuhi siku ya  jumamosi ya mwisho wa mwezi kukamatwa .

Agizo   hilo  amelitoa  leo  wakati  akitoa  salam  zake kwa wananchi wa kata ya  Kalenga  wilaya ya Iringa mara  baada ya  kumalizika kwa shughuli za usafi kwenye Hospitali  teule ya  Iringa .

Alisema  kila  jumamosi ya  mwisho wa mwezi  kila mwananchi atalazimika kufanya usafi katika eneo lake la  biashara  na ni kosa  kufungua maduka ama  biashara  zozote kabla ya saa 3 asubuhi na kutaka wale wote  watakaopuuza agizo hilo kuchukuliwa hatua kali .

Huku  akisema  mbali ya agizo hilo la Rais pia  utekelezaji wa agizo la makamu wa  Rais la wananchi kufanya mazoezi  kwa  ajili ya  kuepuka magonjwa  yasiyoambukizwa  litakuwa endelevu kwa  kila  jumamosi isipo  kuwa  jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni maalum kwa usafi japo   kila  siku  wananchi wanahimizwa  kufanya  usafi maeneo yao.
Wakati  huo huo mkuu  huyo wa mkoa ameliagiza  jeshi la  polisi  mkoa wa  Iringa kuwakamata  ndugu  wa  watoto  waliobakwa    wanaofika vituo  vya  polisi kuwatetea watuhumiwa hao ili  wasamehewe.

Alisema   chimbuko la  ongezeko la  watoto  kuendelea  kubakwa ana kulawitiwa  mkoani hapa  ni tabia ya baadhi ya ndugu  kuwalinda  watuhumiwa  wa matukio ya ubakaji .

Hivyo  alisema   kwa  kuwa  mkoa  umeweka  mkakati  wa  kuwalinda  watoto   dhidi  na vitendo vya  ubakaji na ulawiti  vinavyoendelea  katika maeneo  mbali mbali ni  vema wananchi  wote kuungana  kuwalinda  watoto  hao kwa  kutowatetea  watuhumiwa wa  ubakaji ama ulawiti .

“ Nawaombeni  sana  wananchi  wa  mkoa  wa Iringa kwa   haya  matukio ya  watoto  kubakwa suala la huruma  tuweke kando  tuungane  kuwalinda  watoto  wetu tukiendelea  kuwatetea  watuhumiwa kwa  kuwaonea  huruma  tunaongeza tatizo la  wabakaji na walawiti  hawa  kuendelea  kuwaharibu  watoto  wetu ……kuanzia  sasa  nitamuagiza kamanda wa  polisi  mkoa wa Iringa  ili  kuwaagiza wakuu wa vituo  vya  polisi  vyote ndani ya  mkoa wa Iringa wasikubali  kuwapa  dhamana  watuhumiwa zaidi ya  kuwakamata  ndugu hao  wanaowaonea  huruma  wabakaji hao”

Mkuu   huyo  wa  mkoa ametoa  agizo hilo  ikiwa ni  siku tano  zimepita  toka mtoto  wa darasa la nne shule ya msingi Ipogolo  kubakwa na kaka  yake  Emmanuel Kunzugala (25) na mtuhumiwa  huyo kumtishia  kumuua mtoto  huyo  iwapo angefichua  siri hiyo kabla ya  kukamatwa na  jeshi la polisi  huku  ndugu  wakiandamana  kwa  mkuu wa mkoa kutaka kuomba mtuhumiwa huyo kuachiwa  ili  wamalizane kifamilia.
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  kulia  akishiriki na  wanafunzi  wa chuo   wauguzi (Tosamaganga Nursing) pamoja na  wananchi  wa Tosamaganga  kufanya  usafi  maeneo yanayozunguka  chuo na Hospitali teule ya wilaya ya  Iringa (Ipamba ) leo
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  wa  pili  kushoto na katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu   wakiwa na  watumishi wa Hospitali ya teule ya  Iringa na wananchi leo baada ya  usafi
Viongozi  mbali mbali  kutoka  ofisi ya  mkuu wa mkoa wa Iringa , kata ya Kalenga  na Hospitali ya Ipamba  wakimsikiliza  mkuu wa  mkoa wa Iringa
Wananchi  wa Kalenga wakimsikiliza mkuu wa  mkoa wa Iringa
Wafanyakazi wa Hospitali teule ya wilaya ya Iringa  Suso Vahaya kushoto na Edrose Mwelela  kati  wakifanya usafi nje ya   Hospitali  teule ya  Iringa  leo
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto  akiwa na watumishi wa Hospitali teule ya Iringa  leo
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza akishiriki  kufanya usafi leo  na wanafunzi  wa chuo cha wauguzi Tosamaganga  Iringa
Kazi  ya  usafi  ikiendelea 
Rc  Iringa  Amina Masenza  akifurahi jambo  wakati  akiendelea  kufanya usafiri 
Wanafunzi na  wananchi  wakishiriki  usafi na mkuu wa mkoa wa Iringa  leo
Shughuli ya  usafi wa mazingira  ikiendelea
Mkuu  wa  chuo cha  wauguzi Ipamba  Leon Mgohamwenda kulia akitoka  kuonyesha  eneo ambalo mwanafunzi wa chuo  hicho Tumaini Mtokoma  aling'atwa na nyoka na  kufa
Wanafunzi wa  chuo  cha  wauguzi Tosamaganga  wakiwa katika  usafi leo
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza (mwenye Kilemba cheusi)  akikagua maeneo ya Hospitali  teule ya  wilaya ya  Iringa  leo kabla ya kuanza usafi
Watumishi kutoka  ofisi ya  mkuu wa mkoa wa Iringa na  wale wa Halmashauri ya  Iringa  wakijiandaa kwa  usafi
Rc  na  timu yake   wakielekea katika usafi kwenye mawodi
Usafi  wa  kuweka  sawa  vifaa tiba  vilivyoharibika ukifanyika
Mwitikio  mzuri wa usafi  Iringa
Wananchi  wakiwa katika usafi
Mtumishi wa Hospitali teule ya  Iringa  akigawa  vifaa vya kufanyia  usafi
Wanafunzi wa  chuo  cha  uuguzi  Ipamba  wakiwakatika  usafi  leo
Wanafunzi  wakifurahia  kufanya usafi pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa hayupo  pichani
Usafi  wa Mazingira ukiendelea hospitali teule ya Iringa  leo
Watumishi  wa Hospitali  teule ya Iringa  wakiwa katika usafi wa pamoja na  mkuu wa mkoa wa Iringa leo Picha na Habari na matukiodaimaBlog

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE