March 18, 2017

RC IRINGA ANUSURIKA KUGONGWA NA GARI ASKARI WAWILI WAJERUHIWA AKIWEMO ALIYEJITOSA KUMNUSURU RC KUGONGWA

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza akimtazama  dereva  taxi aliyetaka  kumgonga na gari kabla ya  kuokolewa na askari Antony Mwita  ,askari  wawili  walijeruhiwa katika ajali  hiyo  leo asubuhi 
Taxi  iliyosababisha ajali 
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  wa tatu kushoto akitoa maelekezo kwa askari  waliokuwa wakimsaidia askari magereza Iringa Greety Mwakipesile  aliyegongwa na gari  wakati wa kujiandaa kwa mazoezi  leo asubuhi 
Askari  polisi  Antony Mwita  akiwa amelalachini  baada ya  kugongwa na gari dogo aina ya  Taxi Carina wakati baada ya  kujitosa  kumwokoa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kugongwa na gari  nje ya  ofisi yake  wakati  wakijiandaa kwa  ajili ya  kuelekea  uwanja wa Samora kwa mazoezi  ya  viungo  leo ,askari  wawili  waligongwa na gari hilo huku mkuu  wa mkoa akinusurika ktokana na jitihada za askari  huyo 
Askari  polisi  wakiwa  wamemkamata  dereva Taxi aliyewagonga  askari  wawili  na kumkosa kosa mkuu wa mkoa wa Iringa 
Kijana  dereva Taxi akiwa  chini ya ulinzi wa polisi baada ya  kuwagonga na gari  askari  wawili  mjini Iringa leo asubuhi 
Askari  polisi na  aliyekuwa  mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza  wakimsaidia askari Antony Mwita  aliyegongwa na gari  wakati  akimwokoa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza  kugongwa na gari 
Askari  Antony  Mwita  akisaidiwa  kuingia katika taxi  iliyosababisha ajali ili  kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa  matibabu  zaidi 
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa   Amina Masenza  akimpa pole  askari magereza Greety Ambwene Mwakipesile  aliyegongwa na gari leo asubuhi  wakati  wakijiandaa kuanza mazoezi ya  viungo 
Katibu  tawala  mkoa  wa Iringa Wamoja Ayubu katikati na viongozi wengine  wakitoka  kumtazama majeruhi wa ajali 

Wasamaria  wema  wakimsaidia  askari magereza  aliyegongwa na gari 
Mkuu  wa wilaya ya Iringa  Ricard Kasesela akiwa amechukizwa na ajali  hiyo 
Gari la RC  Iringa  likisaidia  kumkimbiza  hospitali askari  aliyejeruhiwa kwa  ajali ya gari 
Askari  wa  usalama  barabara  wakiingia kwenye gari  lililosababisha ajali ili  kumkimbiza  mwenzao Hospitalini 
.................................................................................................................................................

Na  MatukiodaimaBlog

MKUU  wa  mkoa  wa Iringa Amina  Masenza amenusurika  kifo huku askari  wawili wakijeruhiwa vibaya  akiwemo askari wa  jeshi la  polisi Iringa Antony Mwita  ambaye  alijitosa kumwokoa mkuu  huyo wa mkoa asigongwe na gari  dogo aina ya Taxi  ambalo  liliparamia wananchi  waliokuwa katika maandalizi ya kuanza mazoezi ya  viungo .

Ajali   hiyo  imetokea majira ya  saa 12.25 leo     asubuhi   eneo la  ofisi ya mkuu wa mkoa  na kamanda wa polisi zilizopo kata ya Gangilonga  kwenye  barabara  ya Pawaga Road  baada ya gari lenye namba  za usajili  T 479 CKZ Taxi Carina kuwaparamia  askari  hao .

Wakielezea juu ya tukio  hilo baadhi ya  mashuhuda wa  tukio hilo akiwemo  aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza  alisema kuwa wakati ajali  hiyo  inatokea ailikuwa hatua kama 15  kutoka  eneo la ajali na alishuhudia  gari  hilo  likiwavaa watu hao  ambao  walikuwa kando ya barabara  kwa  ajili ya maandalizi ya kuelekea   uwanja  wa Samora katika mazoezi  ya  viungo .

“ Mimi  na  wenzangu  tulikuwa tunasogea   kuungana na  wenzetu  kwa  kupewa maelekezo na mkuu wetu wa mkoa mheshimiwa Amina Masenza kama  ilivyokawaida  yetu kwa  kila jumamosi  ….wakati tunasogea   kuna  gari dogo  lilitupita  na mbele yetu kulikuwa na gari  ndogo  ambayo  ilikuwa  inakuja kwa  mwendo wa kasi  kwetu na upande wa  kulia kwetu ndiko  walikuwepo  wananchi ambao  wanajiandaa kuanza mazoezi na mkuu wa mkoa  hivyo dereva wa  gari hilo kutokana na uzembe na kukaidi amri ya  askari  wa usalama barabara  ambao  walimsimamisha aliwavaa askari  hao akiwemo askari Anton  aliyekuwa akimnusuru  mkuu wa mkoa”

Kiponza  alisema  kuwa  pasipo  askari  huyo  kumsukuma kwenye  mtaro mkuu wa  mkoa basi  gari  hilo  lilikuwa  linamgonga mkuu wa mkoa  na  kuwa  ni jambo la  kumshukuru Mungu kuepusha madhara  zaidi kwa  wananchi  waliokuwepo  eneo hilo  pia pongezi nyingi kwa askari  huyo kwa  kujitoa mhanga kumwokoa mkuu wa mkoa.

Akitoa  taarifa ya ajali  hiyo  kwa  wananchi  waliofika  uwanja wa Samora  kwa niaba ya  mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  alisema  kuwa  katika ajali  hiyo majeruhi ni  wawili  ambao ni askari  mwanamke  wa jeshi la Magereza Greety  Mwakipesile ambao amevunjika mguu na askari wa  jeshi la  polisi Antony  Mwita  aliyekuwa akimwokoa mkuu wa mkoa kugongwa ambae  ameumia usoni .

Kasesela  alisema mkuu  wa mkoa  yupo salama na amejumuika  mazoezi na  wananchi hao hadi mwisho na  kuwa  mazoezi  yataendelea kwa  ajili ya  kuepuka magonjwa  yasiyoambukiza japo  kwa  siku ya   jumamosi  ijayo mazoezi hayatafanyika na  wananchi  wote  watalazimika  kushiriki  usafi kwa kusafisha maeneo yao ya  biashara kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi na kuwa  siku  hiyo mkuu wa mkoa atapita  kukagua usafi  nyumba kwa  nyumba na jeshi la polisi litatakiwa  kuwakamata wote  watakaofungua maduka mapema.
Aidha  mkuu  huyo wa wilaya  amepongeza jitihada za askari  huyo aliyefanya  jitihada za  kumwokoa mkuu wa mkoa na  kuwapongeza askari walioshiriki kumkamata dereva huyo pasipo kutumia  nguvu  yeyote na  kutaka  wananchi  kuiga mfano huo wa  ukamataji  salama .

Kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa Julius Mjengi  ambae  alikuwepo  katika tukio  hilo alithibitisha  kutokea kwa tukio hilo na kuwa askari  Mwita  aliyepata majeraha  ametibiwa na kuruhusiwa huku askari Mwakipesile  akiendelea na matibabu katika Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa .

Usikose  nakala ya  gazeti la Mtanzania kesho  jumapili 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE