March 20, 2017

RC IRINGA ALAANI MWANAFUNZI LUKOSI SEKONDARI KUBAKWA NA KUTUMBUKIZWA MTONI

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akifungua kikao cha walimu na waratibu Elimu kata katika wilaya ya Iringa leo

MKUU wa Mkoa wa Iringa Amena Masenza amelaani tukio la mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Lukosi wilaya ya Kilolo Kupoteza maisha kwa kutumbukizwa katika Mto baada ya kubakwa. 

Akizungumza leo Katika ukumbi wa Shule ya sekondari Lugalo mjini Iringa kwenye kikao cha pamoja na walimu wakuu na waratibu wa elimu kata kutoka wilaya ya Iringa alisema kuwa tukio hilo la kinyama limemsikitisha Sana na kutaka wananchi kuwafichua wabakaji .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alikutwa na tukio hilo wakati akifua nguo katika mto Lukosi na kuwa mwili wake bado haujapatikana. 

Hivyo alisema kuwa jitihada za wananchi kuendelea kutafuta mwili huo zinafanyika huku akisema kuwa mkoa umejipanga kuendelea na mapambano dhidi ya wabakaji. 

Aidha mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kutowatuma watoto wao baada ya saa 12 jioni madukani na kuepuka kuwalaza wageni chumbà kimoja na wageni. 

"wananchi wa mkoa wa Iringa naomba tushirikiane kukomesha matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto kwa kutowapa nafasi watoto kulala na wageni kwani baadhi ya wageni si wema "

Alisema baadhi ya wazazi mkoani Iringa wanatabia ya kuwachanganya watoto na wageni chumba kimoja na baadhi yao wamekuwa wakiwashusha watoto vitandani na kuwalaza wageni. 

Hivyo alitaka wageni kulazwa sebuleni badala ya kuwalaza katika chumba cha watoto. 

kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la mwanafunzi la mwanafunzi huyo kufariki dunia. 

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi jumapili majira ya jioni wakati mwanafunzi huyo akioga katika mto huo baada ya kumaliza kufua nguo. 

Alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Emeni kisambwa aliyekuwa akisoma kidato cha pili shule ya msingi Lukosi. 

Kamanda Mjengi alisema kuwa mtuhumiwa huyo ambae amekamatwa na jeshi la polisi baada ya kumkuta mwanafunzi huyo akioga alimfuata na kumteka kwa kutaka kumvusha upande wa pili wa mto lakini baada ya kupigiwa kelele na mwananchi aliyekuwa akipita eneo hilo alimwachia mwanafunzi huyo katikati ya mto na kukimbia. 

Hivyo alisema mwili wa mwanafunzi huyo unatafutwa na uwezekano wa kumpata akiwa hai haipo. 

Alisema mtuhumiwa huyo Mhidini Kikunile(35)amekamatwa na polisi na kukubali kuhusika na tukio hilo. 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE