March 23, 2017

RC AAGIZA KIJANA ALIYEMBAKA MDOGO WAKE WA MIAKA 13 KUPIMWA UKIMWI


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akifundisha leo mjini Iringa
....................................................................................
Na matukiodaimaBlog

SERIKALI mkoa wa Iringa imeagiza mkazi wa Ipogolo Emmanuel  Kuzungala (25)ambae anatuhumiwa kumbaka mdogo wake wa miaka 13 kupimwa virusi vya ukimwi na iwapo itabainika ana maambukizi basi kufunguliwa kosa la pili la kuambukiza UKIMWI kusudi. 

Kuwa mbakaji huyo alimtishia kumchinja mtoto huyo iwapo angefichua Siri ya kubakwa kwake. 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara katika shule za Kanda ya Ipogolo ambako mwanafunzi huyo alibakwa. 

Alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kijana huyo kumbaka mdogo wake huku ndugu zake kuonyesha kuficha tukio hilo. 

"sipendi kuona matukio haya ya ubakaji yanaendelea kutokea mkoani kwangu ni juzi tu mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya msingi Lukosi Kilolo kabakwa na mwili wake kutupwa kwenye mto na jana mwili huo umepatikana na amezikwa.... Sasa haya matukio nitaendelea kupambana na naomba wananchi fichueni wabakaji "

Aidha mkuu huyo alisema watuhumiwa wote wawili wa ubakaji wamekamatwa na huyu aliyebaka mdogo wake wa miaka 13 mwanafunzi wa darasa la nne nimeagiza apimwe afya yake. 

Kuwa lengo la kuaiza apimwe VVU ni kutaka kujua kama kamuambukiza VVU ili mbali ya kesi ya ubakaji kuongezwa kesi ya kumwambukiza UKIMWI kusudi. 

Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa ameagiza walimu wa shule za msingi ukanda wa Ipogolo kuwachunga wanafunzi na vitendo vya ubakaji kutokana na ukanda huo kuongoza kimkoa kwa matukio ya uvutaji bangi na pombe. 

Aidha mkuu huyo amemwagiza afisa elimu mkoa wa Iringa kuandika barua ya kuwapongeza walimu wa madarasa ya Kwanza katika shule za msingi Manispaa ya Iringa kutokana na ofisi yake kufurahishwa na uwezo wa wanafunzi katika kujua kusoma kuhesabu na kuandika. 

Alisema amejionea mwenyewe kwa kuwapima wanafunzi hao kwa kuingia madarasani kufundisha na kweli wanafunzi wapo vizuri Sana. 

Huku akitaka mratibu wa elimu kata ya Ruaha kutimiza wajibu wake vinginevyo ajitumbue mwenyewe. 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE