March 2, 2017

RC AAGIZA HALMASHAURI KUANZISHA MAJUKWAA YA UWEZESHWAJI WANAWAKE KIUCHUMI

Mkuu  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akizindua  jukwaa la  uwezeshaji wa  wanawake  kiuchumi  ngazi ya mkoa  leo katika  ukumbi wa Siasa ni  kilimo
Wajumbe   wa jukwaa hilo  wakiwa katika  uzinduzi
Mstahiki meya wa Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe wa pili  kulia  akiwa katika  uzinduzi wa  jukwaa la  wanawake kiuchumi
Mbunge wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa Ritta Kabati  akiwa katika uzinduzi wa  jukwaa la uwezeshaji wanawake  kiuchumi ngazi ya  mkoa
Na MatukiodaimaBLog
SERIKALI  mkoani  Iringa  imezitaka  halmashauri  zote  za  wilaya katika  mkoa  huo  kuhakikisha  zinakamilisha  uchanguzi wa wenyeviti wa baraza la uwezeshaji wanawake  kiuchumi   kama njia ya  kufaidika na  fursa  mbali mbali  kupitia baraza  hilo .

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa  jukwaa la  uwezeshwaji wa  wanawake  kiuchumi  ngazi ya  mkoa leo  katika ukumbi wa Siasa  ni  kilimo  mkuu wa mkoa wa Iringa  Amina  Masenza  alisema  kuwa  uanzishwaji wa baraza  hilo  ni utekelezaji wa agizo la  serikali  ngazi ya  Taifa   hivyo ni wajibu wa  kila wilaya  kuhakikisha  inaunda  baraza  lake na  kuwa  na uongozi kamili .

Alisema  kuwa  lengo la  serikali  kuanzisha   jukwaaa  la   kuwawezesha  wananchi wake  kiuchumi na  kuondokana na  uchumi  wa kubahatisha na  kuwa na uchumi   imara  na  shirikishi , kuwa katika  jukwaa  hilo makamu wa Rais  mama  Samia  Suluhu  ni  mmoja kati ya  wajumbe  wa  baraza la wanawake la  uchumi  duniani  jambo  ambalo  wao kama  wanawake  wanampongeza kwa  kuwepo katika nafasi hiyo .

“ Katika  kuleta  ufanisi  kwenye utekelezaji mheshimiwa makamu  wa Rais  ameelekeza kuwepo kwa majukwaa la  wanawake kiuchumi katika  mikoa  yote na  wilaya  zote za  Tanzania  na  kuwa kazi kubwa ya  majukwaa hayo  yatasaidia  uelewa zaidi wa wanawake  katika masuala mbali mbali yakiwemo ya  kibiashara , uwekezaji  ,upatikajani wa mitaji  , sheria  za nchi na fursa nyingine   nyingi “

Alisema  kuwa  utekelezaji wa majukumu hayo  utafanyika  kwa  kushirikiana na  taasisi mbali mbali zikiwemo za  tawala  za mikoa  ,serikali za mitaa na nyingine  kwa  mujibu wa taratibu ambazo  zimeelekezwa na makamu wa Rais .

Hivyo  alisema kwa  upande wa mkoa  wa Iringa  umejipanga  kuendelea  kuandaa majukwaa ya wanawake ya kuwawezesha kiuchumi  kila  baada ya  miezi  sita na kazi kubwa ya  majukwaa hayo  ni kutoa mafunzo mbali mbali kwa wanawake  ndani ya  mkoa.

Mkuu  huyo  wa  mkoa  alisema  jukwaa  hilo  litakuwa ni jukwaa shirikisho kwa  sekta za umma na  bifasi na  hivyo anawaomba  wanawake  wote  mkoani hapa  kutumia jukwaa  hilo  bila  kujiweka  nyuma ya jukwaa huku  akiwataka  wanaume  wote  kuhakikisha  hawapo nyuma ya  jukwaa hilo.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE