March 13, 2017

RAIS DKT.MAGUFULI AKUTANA NA RAIS DKT.SHEIN IKULU DODOMA

LUMU 2
Ikulu,Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Machi 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.
Dkt. Magufuli amesema katika mazungumzo yao wamezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtakia heri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia leo kuwa siku yake ya kuzaliwa.
Kwa upande wake Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.
”Siku ya kuzaliwa ni siku ya furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana  na leo nimefurahi sana” amesema Dkt. Shein.
Dkt.Shein amesema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli ili waweze kubadulishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
13 Machi, 2017

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE