March 15, 2017

POMBE ZA VIROBA KATONI 1,601 ZAKAMATWA NA POLISI IRINGA

Kamanda  wa  polisi  mkoa  wa Iringa (RPC) Julius Mjengi

                                                  Na MatukiodaimaBlog
UTEKELEZAJI  wa agizo la waziri mkuu Kassim Majaliwa  jeshi la polisi  mkoa wa Iringa unaendelea  baada ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kufanikiwa  kukamata  katoni 1,601 za  pombe  ya  konyagi  iliyofungwa katika  vifungishio  vya plastiki maarufu  kwa  jina  la viroba .

Mtanadao  wa matukiodaimaBlog umezungumza na kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa Julius Mjengi  leo  ofisini  kwake  na kusema  kuwa jeshi  lake limekamata  pombe  hiyo  ikiwa ni  mwendelezo  wa msako   ulioanzwa  kufanywa na  jeshi  lake katika maeneo  mbali mbali ya  mkoa wa Iringa .

Alisema  kuwa pombe   hiyo  imekamatwa kwa  wafanyabiashara   wawili  wakubwa katika  neo la Miyomboni mjini  Iringa na Mlandege katika Manispaa ya  Iringa na  kuwa  tayari mzigo  huo  ambao  ulikuwa  umefungiwa ndani baada ya  kupigwa marufuku  upo  chini ya  polisi .

Pamoja na  kukamata mzigo  huo  kwa  wafanyabiashara  wakubwa pia  alisema  Packeti 53 na  na box 2 za  pombe  hiyo ya  viroba vya aina mbali mbali imekamatwa  kwa  wafanyabiashara    wadogo  wadogo katika  maeneo ya Kitanzini , Ipogolo na Igumbilo mjini  Iringa .

Kamanda  Mjengi alisema  kuwa oparesheni  ya  kusaka   wanywaji na  wausaji  pamoja na wasambazaji  wa Viroba  inafanyika matika maeneo mbali mbali ya  mkoa  wa Iringa na  kuwata rai  wema  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa kuwafichua   wanaoendelea  na biashara   hiyo  .

“ Jeshi la  polisi lipo kazini  muda  wote  kuwasaka  wanaoendelea  na matumizi ya  viroba na  kuwachukulia hatua …..hivyo ombi kwa  wananchi wema  ni  kuendelea  kutoa taarifa  za  siri kwa  jeshi la  polisi “

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE