March 10, 2017

NAPPE NAUYE ANASTAILI KUWA WAZIRI MKUU

  JOHN JOSEPH | CHAMPIONI| MAKALA BONGO DAR ES SALAAM: NIMESHASEMA mara kadhaa katika makala zangu za nyuma lakini halitakuwa jambo baya kama nikiligusia leo kidogo kwa msomaji mpya wa makala zangu, kuwa mimi siyo mpenzi wa siasa na sifi kirii kufanya siasa katika maisha yangu, japokuwa natambua siasa ndiyo inayoendesha dunia.
Robo tatu ya maisha yako unayoishi wewe unayesoma hapa yamesababishwa na siasa, amani au machafuko ya nchi au jamii nyingi kwa asilimia kubwa yanasababishwa na siasa.


Hiyo inamaanisha hata kama huipendi siasa lazima ‘uiishi’. Nimeanza na utangulizi huo kwa kuwa nitakachokizungumza hapa kinaweza kutafsiriwa kisiasa lakini uhalisia ni kuwa nazungumza ukweli ambao nimekuwa nikiuona kwa muda sasa:
Tangu wajina wangu, Rais John Joseph Magufuli alipoingia madarakani na kutangaza baraza lake la mawaziri niliona wazi mlengo wake ni kupenda wasomi au watu waliofi ka levo fl ani ya juu kielimu.Katika chaguzi zake za mawaziri, Rais Magufuli alifanya chaguo sahihi katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwa kigezo cha usomi kwa waziri husika hakikuwa kipaumbele kikubwa kama zilivyo idara nyingine, huo ulikuwa uamuzi sahihi kwa kuwa wizara hiyo ni ukweli kuwa inahitaji kuongozwa na mtu ambaye anaweza kuzungumza lugha na wahusika wake wakaelewa na siyo lazima awe msomi.

Siyo kwamba wasomi hawatakiwi lakini utendaji wa waziri wa wizara hiyo, Nape Moses Nnauye ambao amekuwa akiufanya umenivutia na ninaamini kuna mamilioni ya watu ambao wanamuelewa anachokifanya. Achana na madongo yake ya kisiasa ya hapa na pale ambayo ni kawaida kwa mwanasiasa lakini haya machache niliyoyaeleza chini yanaweza kukufanya uamini kuwa Waziri Nape anastahili kupata cheo cha kuwa waziri mkuu wa wizara yake kama cheo hicho kingekuwepo.
Nasema hivyo kwa kuwa tukumbuke majukumu ya cheo chake yalipatikana baada ya Rais Magufuli kuunganisha wizara kadhaa alipoingia madarakani, hivyo mzigo alionao ni mkubwa lakini ameonyesha kuumudu:
ANAISHI MAISHA YA WASANII
Amedhuria mara nyingi matukio ya wasanii, pamoja na hivyo ametoa ushauri mzuri, amekuwa akiwapa moyo wa kupambana, anawaonyesha njia ya kupita na kupata mafanikio.
Amewavumilia mara kadhaa walioonyesha utovu wa nidhamu kwa kuwa wasanii ni wasumbufu, mfano hai ni siku alipotakiwa kumkabidhi bendera Diamond, msanii huyo alichelewa sehemu ya tukio, Waziri Nape alifi ka mapema na kumsubiri kitu ambacho ni dharau kwa kiongozi mkubwa kama yeye lakini alivumilia.
Amefanya ziara mitaani kusaidia masoko ya kazi za wasanii lakini ni wasanii wachache wameonyesha kumuunga mkono.
ANAJUA KUISHI NA VIJANA
Mara kadhaa amejichanganya na vijana mtaani akionyesha sapoti ya mambo kadhaa ya kimichezo na kiburudani na wakati mwingine jukwaani, kitu ambacho ni nadra kufanywa na mawaziri wengine ‘wasomi’.
ANASAPOTI MICHEZO
Najua Rais Magufuli siyo mpenzi sana wa michezo lakini ukweli ni kuwa Nape amekuwa ‘link’ muhimu kati ya serikali na michezo. Amesaidia kutoa hamasa katika timu za taifa hasa soka la vijana ambalo ndiyo msingi wa mafanikio.Kwenye riadha na michezo mingine napo yupo hata kama siyo mjuzi lakini mara kadhaa nimeona akishiriki na kutoa ushauri wa kile anachoona kipo sahihi. Matukio ya kutembelea Uwanja wa Nyamagana na Taifa katika sakata la viti ni mfano wa jinsi alivyo ‘active’.
ANATHAMINI WANAHABARI
Hivi karibuni kulitolewa tamko la kufungwa kwa TV za mtandaoni lakini Nape akapinga hilo kwa kusema huwezi kufungia wakati hakuna sheria, huo ni mfumo hai na aina ya kiongozi anayetambua kile anachokiongoza  pamoja na hofu kubwa iliyopo kwa wanahabari katika serikali iliyopo madarakani, Nape amekuwa mstari wa mbele kusimamia haki za wanahabari na kuwatetea anapoona wana haki na mara kadhaa ameshiriki katika misiba ya wanahabari.
Anapoona kuna wanahabari wanafanya jambo zuri imekuwa kawaida yake kuwapongeza na siyo kusubiri wakosee tu ndiyo azungumze nao. Pia amewatetea wasanii hadharani alipoona wanatendewa ndivyo sivyo.


ANGALIZO KWA NAPE
Pamoja na mazuri yote hayo lakini moja ya udhaifu ambao nauona kwake ni kuwa mara kadhaa amekuwa akitoa ushauri wa mambo kadhaa, namsii sehemu nyingine asitoe ushauri bali atoe maagizo kwa ufupi aongeza kaukali kiduchu na asiruhusu urafi ki ukamuharibia kazi nzuri anayoionyesha.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE