March 17, 2017

MWIGULU AANZISHA SAFARI YA MAFANIKIO SINGIDA UNITED KWA KUMWITA HANS VAN DER PLUIJM


Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba amekusudia kuifikisha pazuri timu ya Singida United kwa kumsajili  liyekuwa kocha wa Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm ambaye amejiunga na klabu ya Singida United iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao.

Hatua hiyo ni kubwa na ya Mafanikio kisoka katika mkoa wa Singida ambao ni moja kati ya zilizopanda pamoja na Lipuli Fc ya Iringa na Njombe mji

Tayari mkoa wa Singida umeonyesha dhamila ya kweli ya kuwekeza katika soka bila kuwepo kwa sintofahamu kama mikoa mingine

Tayari mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata amepongeza jitihada za Mwigulu ambae ni waziri wa mambo ya ndani kwa jitihada hizo na kuwa wanauhakika kufanya vema ligi kuu na kuongeza kwa.

"CCM Mkoa tunaendelea na matengenezo ya uwanja Wa NAMFUA ili kuu game Mkono juhudi hizo. .."

Mtandao wa matukiodaimablog unapongeza jitihada hizo na kushauri mikoa mingine ambayo timu zao zimepanda kuanza kufanya maandalizi na kuachana na mivutano pia kwa zile zisozo na viongozi kufanya mchakato huo mapema kwa maelekezo ya TFF ili kufungua milango ya wadhamini kuwekeza katika klabu husika maana hakuna mdhamini atakaekubali kuwekeza pasipo na uongozi ni sawa na kutupa shimoni pesa zake

Hongereni Singida united, Hongera Mwigulu Nchemba mmeonyesha njia wengine igeni mazuri haya


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE