
Mwanamke wa Misri
anayeaminiwa kuwa mwenye uzito wa juu zaidi duniani akiwa na kilo 500,
amefanyiwa upasuaji wa kupunguza unene chini India.
Msemaji wa
hospitali ya Saifee mjini Mumbai amesema kuwa Eman Ahmed Abd El Aty,
mwenye umri wa miaka 36, amepungua kilo 100 baada ya upasuaji." Tunajaribu kumuwezesha kuwa mwenye nguvu za mwili kuweza kusafiri nyumbani Misri haraka iwezekanavyo," ilieleza taarifa ya hospitali.
Familia yake ilisema kuwa hajawahi kuondoka nyumbani kwao kwa miaka 25 hadi siku aliposafirishwa hadi India mwezi Januari kwa ndege.
Msemaji wa hospitali ya Saifee ameiambia BBC kuwa anaweza kupungua kilo za mwili zaidi katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo.
Upasuaji huo ulifanywa na kundi la madaktai walioongozwa na daktari bingwa wa upasuaji wa kupunguzunene wa mwili, Dkt. Muffazal Lakdawala.
Upasuaji wa kupunguza uzito na unene wa mwili unaofahamika kama -Bariatric surgery, kwa lugha ya kitaalam hutumiwa kama suluhu la mwisho kumtibu mtu ambaye ana uzito unaohatarisha maisha yake.

Wakati alipofikia umri wa miaka 11, uzito wake ulikuwa umeongezeka haraka na akapata kiharusi, hali iliyomfanya kuishi kitandani.
kwa sasa anahudumiwa ma mama pamoja na dada yake.
Hata hivyo Dkt. Lakdawala aliiambia BBC mwezi Disemba kwamba anaamini Bi Abd El Aty hana ugonjwa wa matende bali anaumwa unene wa kupindukia unaosababishwa na kuvimba kwa miguu.
Upasuaji wa bariatric unafanyika vipi

Aina mbili zinazofanyika mara kwa mara za upasuajiwa kupunguza uzito wa mwilini ni:
- Gastric band, upasuaji ambao hufanyika kuzuwia ukubwa wa tumbo ili kiasi kidogo cha chakula kiweze kumshibisha mtu
- Gastric bypass, huu ni upasuaji ambapo mfumo wa kusaga chakula hubadilishwa na kuufanya kupokea chakula kidogo tu cha kusaga na hivyo chakula kidogo ndicho huruhusiwa kusagwa ili kumfanya mtu kuhisi ameshiba.
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE