March 3, 2017

MWAMOTO ATEMBELEA ENEO LA AJALI KIDABADA AMTAKA MHADISI KUTEMBELEA MAENEO KOROFI

Mbunge wa  Kilolo  Venance Mwamoto  akiangalia basi linalofanya safari  zake kati ya mjini  Iringa  na Kidabaga  lililotumbukia mtoni baada ya  kushindwa  kupanda mlima  kutokana  na  mvua  kubwa kuharibu barabara  katika  ajali  hii  mtu mmoja  alipoteza maisha
Diwani wa kata ya Ng'uruwe  Pancras Kihanga  kulia akiwana mbunge Mwamoto  kumuonyesha maeneo korofi ya  barabara
Mwamoto akiwa na watoto wa kata ya Ng'uruwe
Mwamoto  akikagua  ujenzi wa nyumba ya  madaktari  kituo  zahanati ya Masisiwe
Mazao yakiwa  ymestawi  vema  Kilolo
 
Na MatukiodaimaBlog
 
MVUA   kubwa  zinazoendelea  kunyesha wilayani  Kilolo  mkoani  Iringa  zimeendelea  kusababisha  kero kubwa kwa  watumiaji wa barabara  za  wilaya  hiyo kwa  malori linayofika  kubeba mazao kukwama huku mtu mmoja akipoteza maaisha kufuatia basi la kampuni ya  upendo kutumbukia mtoni  baada ya  kushindwa  kupanda mlima.

Wakitoa kero  zao  kwa mbunge wa  jimbo la  Kilolo  Venance Mwamoto  aliyefanya ziara ya  ukaguzi wa miundo mbinu katika kata ya Kidabaga na Ng'uruwe  jana  wananchi hao   wakiwemo madereva  waliokwama kwa zaidi ya siku mbili katika  eneo la  Kidabaga   walisema  kuwa  hali ya mvua  inayoendelea  kunyesha  imeendelea  kuwatesa na hivi sasa  wanalazimika  kulala njiani   hasa mvua  zinaponyesha  wakiwa  njiani .

Yohana  Sanga  ni  mmoja kati ya  wasafirishaji  wa mazao ya  misitu  katika  wilaya ya  Kilolo  alisema  kuwa   kutokana na mvua  hizo  hivi sasa  sehemu kubwa ya  barabara  za  wilaya ya  Kilolo  zimekuwa  hazipitiki  kirahisi hivyo  kuiomba  serikali ya  wilaya ya  Kilolo  kuangalia   uwezekano wa  kuboresha maeneo korofi  ambayo yamekuwa hayapitiki  hasa kipindi cha mvua .

Alisema  kutokana na hali hiyo hasa sasa  tayari  mwanamke mmoja amepoteza maisha na  wengine zaidi ya  watano ni majeruhi  baada ya  basi  walilokuwa wakisafiriki  kuelekea  mjini  Iringa  kushindwa  kupanda mlima wa Kidabaga na  kuporomoka  mtoni .

Diwani  wa kata ya  Ng'uruwe Pancras Kihaga  ambaye aliongozana na mbunge  huyo  kukagua  maeneo korofi ya barabara za Kilolo  alisema  kuwa maeneo ambayo yanawatesa  wasafiri na  wasafirishaji  ni pamoja na Kidabaga  na baadhi ya maeneo ya  kata  ya Ng'uruwe na  hivyo  kumuomba mbunge huyo  kusaidia  kufikisha kilio  hicho kwa  Halmashauri ya  Kilolo .


Mbunge  Mwamoto  mbali ya  kuwapa pole  wahanga  wa  tukio la ajali ya  basi na  ndugu  wa mkazi wa jimbo hilo aliyepoteza maisha kwa ajali ya  basi bado alimtaka  mhandisi wa ujenzi katika Halmashauri ya  Kilolo  kutoka ofisini na  kutembelea  barabara   hizo ili  maeneo korofi kuyafanyia kazi haraka badala ya  kusubiri maafa .


Alisema  shida iliyopo ni  uwajibikaji mbovu wa  mhandisi wa  ujenzi kila  wakati  amekuwa  akingoja  kusukumwa ndipo  atoke  ofisini jambo ambalo  linapelekea wananchi kuendelea  kuilalamikia  serikali  kwa kila  changamoto inapojitokeza .


Mbunge huyo  alisema kwa sasa ukarabati wa  eneo hilo  korofi la Kidabaga na  Ng'uruwe  unaanza mara moja  leo ili  kuwezesha  wananchi kupata mawasiliano ya  barabara  ya  uhakika .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE