March 19, 2017

MWAKALEBELA NJIA NYEUPE UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

Mwenyekiti wa taifa wa Ccm rais Dkt Magufuli akimkabidhi ilani ya Ccm Mwakalebela wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015

Frederick Mwakalebela akiomba kura
..........................................
Na Matukiodaimablog
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini aliyesalitiwa naviongozi wa CCM waliotumbuliwa Frederick Mwakalebela amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

mwakalebela alichukua fomu leo Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma na kueleza kuwa  kuwa sasa umefika wakati wa kuwatumikia watanzania kupitia bunge hilo kwanitakuwa teyari kuwatumika watanzania kwani anazijua changamoto za EAC. 

"umefika wakati wa kuwatumikia watanzania kupitia bunge hili ,uwezo wa kuwatumikia ninao na changamoto mbalimbali za EAC nazijua"alisema Mwakalebela na kuongeza kuwa

"Nawaomba wabunge kunipa ridhaa,kikubwa ni fursa zilizopo Afrika Mashariki na jinsi gani Tanzania itafaidika,naamini CCM inanifahamu Nina imani wataniangalia ili niweze kuwatumikia"

Aidha alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Dk John Magufuli kwa kauli yake ya kutaka wapatikane viongozi waadilifu wasiotumia rushwa na kwamba anaamini uchaguzi huo utakuwa huru na haki. 

Mwakalebela ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM alisema "Uadilifu wangu unajulikana kwani nimefanya kazi sehemu nyingi  nina uzoefu wa kutosha nikifanikiwa kupata nafasi hii sitawaangusha walionichagua na watanzania kwa ujumla "

mwakalebela amechukua fomu hiyo akiwa ni mmoja wa makada na viongozi wenye sifa kubwa kutumikia wananchi kwani alifanya vema TFF akiwa katibu mkuu piá wilaya ya Wang'ombe akiwa mkuu wa wilaya na ni kiongozi msikivu asiye na majivuno 

Ombi kwa wabunge wa Afrika Mashariki tuchague mbunge Makini Mwakalebela kwa faida ya Tanzania na Afrika Mashariki

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE