March 1, 2017

MKUU WA MKOA IRINGA AWATAKA WENYEVITI WA BODI ZA SHULE AMBAO NI WATUMISHI WA UMMA KUJIUZULU NAFASI HIZO

Mkuu  wa  mkoa   wa Iringa Amina Masenza katikati  akiwa na  viongozi mbali mbali akiwemo DC  Iringa Richard Kasesela  kulia  wakitembelea  shule  maalum ya Msingi Mapinduzi 
RC  Iringa  Amina Masenza  akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea  shule ya sekondari Nduli
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia  na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  wakikagua maendeleo ya  wanafunzi  shule ya sekondari Nduli
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  akipokelewa na viongozi wa kata ya  Gangilonga  alipotembelea shule ya msingi Mapinduzi
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa  akikagua  ujenzi wa  vyumba  vinne  shule ya  Msingi Mapinduzi
DC  Iringa  Richard Kasesela  akitoa utambulisho wa viongozi mbali mali wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa shule ya  msingi Mapinduzi
Na MatukiodaimaBlog

MKUU   wa mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza ameagiza  watumishi  wote  wa   serikali  waliochaguliwa  kuwa  wenyeviti  wa  bodi  za  shule  kujiuzulu  mara  moja  nafasi   zao  ili  kupisha  watu  wasio  watumishi kuongoza  nafasi  hizo.
Akizungumza  jana  baada ya  ziara yake ya  kukagua  shule maalum  ya Msingi Mapinduzi  iliyopo kata ya  Gangilonga  mjini  hapa ,alisema  kuwa  baadhi ya mambo shule  hapo  yamekwenda  kinyume na taratibu  kutokana na aliyekuwa  mtendaji  wa  kata  hiyo kuwa  ni  mwenyekiti  wa  bodi ya  shule .

Alisema   kuwa  hajapendezwa na utaratibu wa  uendeshaji  wa shule  hiyo  hasa  katika ujenzi  wa  vyumba  vya madarasa mane  unaoendelea katika   shule  hiyo na hivyo  kuagiza  ukaguzi wa mapato  na matumizi  ya  fedha  katika  shule  hiyo  kufanyiwa  ukaguzi  kwa  kipindi cha  miaka  minne kabla ya  ofisi yake  kuchukua  hatua kwa  wahusika  iwapo  itabainika  kufanya   ufisadi wa  fedha   hizo.

Kuwa  hajafurahishwa na  matumizi ya  fedha  kiasi cha  Tsh milioni 98  zinazotumika  kujenga  vyumba   vinnne  vya madarasa  katika   shule  hiyo na  kuwa  majengo hayo yamejengwa   chini ya  kiwango  kwa thamani ya   pesa  iliyotumika  kutolingana  na ubora  wa majengo  na  hivyo  Pamoja na  kufanya  ukaguzi wa mahesabu bado idara ya ujenzi  Manispaa ya  Iringa  inapaswa  kukagua  ubora  wa majengo hayo .

“ Mtendaji  wa kata  ni msimamizi  wa  shughuli  zote  za  serikali  ngazi ya kata   yake  hivyo  kitendo cha aliyekuwa mtendaji  wa kata  hiyo Mlole Ngwada  kuwa  mwenyekiti wa  bodi ya  shule  ni ukiukwaji wa  taratibu  za  bodi za  shule kimsingi hakupaswa  kuwa mwenyekiti wa  bodi …… kwa  kuwa tayari  amejiuzulu  nilitaka  leo  hapa kama  angekuwa bado ni  mwenyekiti  wa bodi  ningemsimamisha “

Masenza  alitaka  shule  hizo za mkoa  wa Iringa  ambazo bado  wenyeviti  wao  ni  watumishi  wa umma basi kuachia nafasi hizo ili  kutoka nafasi  kwa  bodi  hizo kuwa  huru .
Katika   hatua  nyingine  mkuu  huyo wa  mkoa  aliwataka  wataalam  wa Halmashauri ya  Manispaa y a Iringa  kufanya kazi  za  kitaalam  pasipo  kujishughulisha na  siasa kuwa  siasa  wanachiwe  wanasiasa na wao  kama  wataalam   kufanya kazi za  kitaalam .

Awali mkuu  wa  shule ya Mapinduzi   Clayton  Chungu  alimweleza  mkuu  wa  mkoa kuwa BOQ  iliyotolewa na Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa kwa  ajili ya ujenzi  wa vyumba   hivyo vinne vya madarasa  ilikuwa ni ya  Tsh  zaidi ya  milioni 111  ila  wao  kupitia  bodi ya  shule  waliamua  kubana matumizi kwa  kumtafuta  fundi  wa  kujenga majengo hayo kwa Tsh  milioni 98  na  kuwa sehemu ya   fedha  zozo ni makusanyi ya ada kwa  wanafunzi  ambapo  kila mwanafunzi katika   shule hiyo  ada  yake ni kati ya  Tsh 200000.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE