March 14, 2017

MKOA WA IRINGA WATOA MOTISHA KWA WALIOFANYA VIZURI KWA TOHARA

mratibu wa afya ya mama na mtoto mkoa wa Iringa Mariam Mohamed akimkabidhi katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu kulia keki kwa Aili ya kituo cha Afya Ipogolo kilichofanya vema zoezi la tohara, hafla hiyo imefanyika leo ukumbi wa Ras.

...................................................................
Mtayarishaji wa keki akiiandaa 
Wafanyakazi  wa  idara ya  afya  Manispaa ya  Iringa 
mratibu wa afya ya mama na mtoto mkoa wa Iringa Mariam Mohamed akimkabidhi katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu kulia keki kwa Aili ya kituo cha Afya Ipogolo kilichofanya vema zoezi la tohara, hafla hiyo imefanyika leo ukumbi wa Ras.

.Na MatukiodaimaBlog,Iringa
 MKOA wa   Iringa umetoa motisha mbali mbali kwa kituo cha afya Ipogolo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Hospitali ya rufaa yamkoa wa Iringa baada ya kuongoza kwa kuwafanyiatohara (mikono ya sweta) watoto 1000


 Mratibu wa afya ya mama na mtoto mkoa wa Iringa Mariam Mohamed akitoa taarifa ya zoezi hilo la tohara mkoani hapa kabla ya kukabidhi zawadi hizo leo wakati wa hafla ya hiyo kwenye ukumbi wa katibu tawala wa mkoa wa Iringa ,alisema wamelazimika kutoa motisha hiyo ili kuwapa moyo wa kufanyakazi kuongeza juhudi zaidi

‘’Wizara ya Afya kwakushirikiana na Uongozi wa mkoa wa Iringa kupitia Idara ya Afya na Shirika laJhpiego walianza kufanya utafiti (pilot) wahuduma za tohara ya watoto wachangaTanzania katika Mkoa wa Iringa tangu mwaka 2013 kwa Malengo yafuatayo.. Usalama (Safety) wahuduma za toharaya watoto wachanga Kukubalika kwa huduma(Acceptability)za tohara ya watoto wachanga katika Jamii, Uwezekano (Feasibility) wakutoahuduma za tohara ya watoto wachanga katika vituo vya kutolea huduma kwa kutumiarasilimali zilizopo bila kuongeza gharama au kuathiri huduma zilizopo katikakliniki zilizoainishwa nazo ni CTC,RCH NA WODI YA UZAZI’’


 Hivyoililazimika wauguzi kwenda wizarani pamoja na watumishi wengine ambapo kufuatia kukaa pamoja na kueleza namna itakavyofanyika mwaka 2013  kuwa ni vema kuanza kwa kutumia madaktarikabla ya moja kati ya madaktari kwenda Afrika ya kusini kujifunza .

 Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya mkuu wa mkoa waIringa Amina Masenza ,katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alisema kuwa kwa kuwa hivi sasa mkoa wa Iringa una jumla ya vituo 16vinavyotoa huduma za Tohara ya watoto wachanga. Tangu 2013 mpaka February,2017, jumla ya watoto 6,374 wametahiriwa bila kupata matatizomakubwa.Katika kipindi hiki chote ni watoto 11 tuwame ripoti wakupata madharamadogo madogo ambayo yalitibiwa na kupona kabisa kwa ufanisi katika vituohusika.

 ‘’katika tukio la leonawapongeza na kuwapa motisha watoa huduma na viongozi wa Hospitali ya Rufaa yaAliwataka watumishi kufanya kazi kwaweledi na kwa bidii zaidi ili kuendeleza huduma hiyo na kuwa mfano katika jamiikwa kufanya kazi kwa bidii ,nidhamu na kuwa mfano kituoni na jamii kwa ujumla  

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE