March 15, 2017

MJENGONI BANDI KUFANYA UZINDUZI RASMI MARCH 16 KATIKA UKUMBI WA KLABU HOUSE TRIPLE A

 wanamziki wa bendi ya mjengoni wakiwa wanafanya mambo ndani ya jukwaa la kiwanja cha nyumbani mjengoni Klabu</ span>

Rais wa bendi ya mjengono


Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Bendi mpya  ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni   classic & nbsp; band inatarajia kufanya  utambulisho   wao rasmi kwa mara ya kwanza  mapema  march 16 katika ukumbi wa Triple A klabu house uliopo ndani ya jiji la Arusha


Akiongea na waandishi wa habari  Rais wa bendi hiyo Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa  pamoja kuwa bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani katika uwanja wa nyumbani mjengoni Klabu pamoja na sehemu nyingine mbalimbali lakini walikuwa awajaizindua rasmi  hivyo wanatarajia kufanya uzinduzi ramsi katika siku hiyo ya alyamisi.


Alisema anapend akuwakaribisha wapenzi wote wa muziki wa dance wazee kwa vijana kuja kuona jinsi bandi hii inavyofanya kazi na jinsi bandi hii inavyotoa burudani kwa mashabiki wake huku akisisitiza waje waone staili mbalimbali za mziki zinazochezwa na  wanamuziki wa bandi ya mjengoni


Kwa upande wake  mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdenye& nbsp; alisema kuwa bendi yake imeimarika na wanamziki wanajiamini na ndio maana wameamua kufanya uzinduzi kwa mara ya kwanza rasmi ili wakazi wa mkoa wa Arusha  waweze kuaidi mziki wa dance wenye viwango.


Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa jiji la Arusha wenyeji na wageni pamoja na wale wanaotoka katika mikoa ya jirani kuhuthuria onyesho hilo  kwani bendi yake imejipanga kuwapa burudani ya nguvu ambayo itaacha historia kwani show ambayo wataifanya amna bendi ingine yeyote imeshawai kufanya kama hiyo.


Alisema kuwa bendi hiyo imejipanga kuanza kutoa burudani majira ya saa moja usiku adi majogoo  ,yote hiyo ni kuakikisha wapenzi wa mziki wa dance wanacheza adi pale hamu yao itakapo isha

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE