March 8, 2017

MFANYABIASHARA WA VIROBA AJIPIGA RISASI BAADA YA KUKAMATWA
Mfanyabiashara wa vinywaji mkoani hapa Festo Msalia amejiua kwa kujipiga risasi kichwani usiku wa kuamkia leo kwa kile kinachodaiwa ni baada ya kukamatwa na shehena kubwa ya viroba.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Msalia alifariki jana saa 5.00 usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Amesema marehemu aliondoka nyumbani kwake kwa kutumia gari aina ya Prado na kwenda kujipiga risasi katika eneo la Veyula nje kidogo ya mji wa Dodoma.
"Tulipata taarifa ya kujipiga risasi jana saa 3.00 na polisi walipokwenda waliokota maganda matano katika eneo la tukio na walipompeleka hospitali hawakuweza kuokoa maisha yake kwa sababu alikuwa amejichana chana na risasi, "amesema.
Alipoulizwa kama kifo hicho kunatokana na sakata la ukamataji wa viroba, Mambosasa amesema anafikiri suala hilo ni hisia tu kwasababu marehemu alikamatwa Machi 3 mwaka huu akiwa na shehena ya tani 1.5 za pombe ya viroba.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE