March 5, 2017

MAZOEZI YA VIUNGO JUMAMOSI YA MACHI 4 , RC IRINGA ,DC MUFINDI NA IRINGA WASHIRIKI KUFANYA MAZOEZI NA MVUA

Viongozi  mbali mbali wa  mkoa wa Iringa  wakishiriki kufanya mazoezi na  mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (wa tatu kulia)  kushoto wa kwanza ni katibu tawala wa  mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela , mbunge wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa Ritta Kabatti  na  wa nne kutoka kulia ni mkuu  wa mkoa wa Iringa  wakiwa katika mazoezi ya  viungo katika  uwanja wa Samora jana  huku mvua  ikinyesha
Watoto   hawa  ambao ni watoto pekee  kufika katika mazoezi asubuhi  wakijumuika na viongozi  mbali mbali wa  mkoa  kufanya mazoezi
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza wa pili kulia akiwa katika mazoezi  ya  viungo kwa afya
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akifurahi na  watoto  wakati wa mazoezi  uwanja wa  Samora  jana
Mkuu  wa  wilaya ya  Mufindi Jamhuri  Wiliam wa  tatu  kulia na katibu tawala wa  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayubu wakiwa katika mazoezi  wa pili  kushoto ni  mbunge wa Kilolo  Venance Mwamoto
Mkuu wa wilaya ya Mufindi  Jamhuri  Wiliam kulia akishiriki mazoezi katika  uwanja wa  Samora  jana  na wananchi mbali mbali  wa  pili  kushoto mbunge wa  Kilolo Venance  Mwamoto
Mtumishi wa ofisi ya  mkuu wa  mkoa  wa Iringa  LImbaksye  Shimwela  akiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya  Iringa Dr Wiliam kulia  wakifanya mazoezi
Mkuu wa chuo  kikuu cha  Iringa Prof Joshua Madumulla kushoto akishiriki mazoezi
watumishi  ofisi ya RC  Iringa wakiwa katika mazoezi
mwalimu  wa soka timu ya polisi Iringa Sarehe  akifurahia mazoezi
Maofisa  habari Manispaa ya  Iringa  Sima Bingileki  kulia na Janeth Matondo wakijumuika katika mazoezi
Maofisa  wa  polisi na  askari  wakiwa katika mazoezi  ya pamoja uwanja wa Samora
DC  Kasesela  kulia na mbunge Kabati  wakiwa katika mazoezi
RC Iringa wa  pili kulia  akifanya mazoezi mazito


MKUU  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza amesema  kuanzia sasa  kila jumamosi ni  siku ya  mazoezi  na upo  uwezekano  wa hadi jumamosi ya  siku ya  usafi ambayo ni  jumamosi ya  mwisho wa mwezi kabla ya  usafi  wananchi  wake  kushiriki mazoezi na baada ya  mazoezi  watafanya usafi  eneo  lililoteuliwa kwa  wiki  husika .


Alisema  ni vema kila mwananchi wa  mkoa  wa Iringa  kujenga  utamaduni wa kushiriki mazoezi hayo ambayo yanafaida  kubwa kwa afya  zao hasa katika  kukabiliana na magonjwa  yasiyo ambukizwa .

Mkuu  huyo wa  mkoa  aliwapongeza wananchi  waliojitokeza jana kufanya mazoezi  huku  mvua ikinyesha na kuwa hakutegemea kuona umati mkubwa wa watu  kushiriki mazoezi na  mvua  hiyo  hivyo  kuwaomba  wakuu wa  vyuo mkoani hapa   kuwahamasisha  wananzi  wao kushiriki katika mazoezi hayo ya pamoja .


Alisema mazoezi  hayo huanza ofisini  kwake  kila  jumamosi kuanzia majira ya saa 12 ;00 asubuhi  kuelekea katika  uwanja  wa michezo wa  Samora ambako  mazoezi ya viungo  hutolewa na  wataalam  kutoka  vituo  vya mazoezi  waliopo mkoani Iringa .


Katika mazoezi  hayo  mkuu wa  wilaya ya  Mufindi Wilima Jamhuri  alipata  kujumuika na  kuuomba  mkoa  kutenga  jumamosi moja  ya mwezi kwenda  kushiriki mazoezi kama  hayo wilayani Mufindi kama  sehemu ya  kuwahamasisha  wananchi wa wilaya ya  Mufindi  kujitokeza kwa wingi katika mazoezi ya  viungo .


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE