March 2, 2017

MASHINE ZA KUTENGENEZA VIROBA ZAKAMATWA

mon1
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha na kutengeneza pombe kali(viroba)  na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.
mon2
Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni  hiyo pasipo kufuata kanuni za TFDA wala pasipo kuweka stika za TRA.
mon3
Mrundikano wa maboksi uliopo kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.
mon4
Mashine zinazotumiwa na kiwanda cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya viroba pamoja na kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE