March 16, 2017

MARUFUKU MPYA YA TRUMP YAGONGA MWAMBA
Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine tena, amekumbana na wakati mgumu, katika juhudi zake za kupinga sheria za uhamiaji dhidi ya mataifa yenye Waislamu wengi duniani.

Hii ni baada ya hakimu wa Mahakama Kuu iliyoko Hawaii, kuzuia marufuku hiyo ya Rais, kabla ya kuanza kutumika rasmi.

    Trump hajui apeleke wapi mshahara wake

    Maswali magumu kuhusu marufuku ya Trump

Amri hiyo kuu ya Rais kwa kiasi fulani, ilikuwa imewazuia wakimbizi na wahamiaji kutoka mataifa kaadhaa kuingia Marekani.

Bwana Trump ameelezea uamuzi huo wa mahakama, kuwa wa kushangaza na ambao haujawahi kufahamika awali, na ameapa kupeleka kesi hiyo hadi katika mahakama ya juu zaidi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE