March 16, 2017

MANJI KUPANDISHWA KIZIMBANI TENA LEO KWA TUHUMA ZA MATUMIZI YA HEROINE

Kesi inayomhusu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ya juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine, inatarajiwa kusikilizwa tena  Alhamisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuahirishwa kwa mara ya mwisho Februari 16, mwaka huu.
 
Manji anatuhumiwa kutumia madawa hayo kinyume na sheria ya mwaka 2015 ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) namba 5 ambapo inadaiwa Manji alitumia dawa hizo Februari 6 na 9, mwaka huu.
 
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Osward Tibaloyekomya huku upande wa Manji ukiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa.
 
Baada ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kesi hiyo, Manji alikataa mashtaka hayo na kuachiwa nje kwa dhamana ya milioni 10 iliyotolewa na Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa.
 
Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kusikilizwa kwa kesi hiyo bila ya Manji kuwepo kutokana na kuumwa kwani kwa sasa amelazwa kwenye Hospitali ya Aga Khan ambapo anasumbuliwa na tatizo la moyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE