March 28, 2017

MAMA ALIYEUNGUZWA NA MAJI YA MOTO AMSHUKURU RAIS DKT MAGUFULI


Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli. Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea kuchukua jukumu la kumsaidia.Mkuu wa Jengo la Sewahaji Bibi. Salome Mayenga (kushoto) na Mkuu wa Wodi namba 24 Sewahaji, Muhimbili Bibi. Georgina Kabaitileki.
Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli. Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea kuchukua jukumu la kumsaidia.
Mkazi wa mkoa wa Mara ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa mgonjwa kufuatia majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi,Bibi. Neema Mwita akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kwa kitendo chake cha kumfariji na kumsaidia kupata matibabu ya hayo wakati akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.  Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma

 ........................................................

Na. Georgina Misama MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa moyo wake wa kujitoa na kuwajali wanyonge hasa wagonjwa wasiojiweza na wenye uhitaji  wa gharama za matibabu.

Hayo yamesemwa leo na Bi. Neema Mwita Wambura maarufu kama ‘Mgonjwa wa Magufuli’ wakati alipotembelewa na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwaajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata majeraha ya moto.

“Ninamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli kwa msaada wake katika matibabu yangu. Hivi sasa mimi nina maendeleo makubwa, naweza kuongea, kula na hata kugeuza shingo yangu. Nitamuombea Rais Magufuli mpaka siku naingia kaburini, Mungu ambariki” anasema Neema.

Akisimulia mkasa uliompata Neema anasema kwamba alimwagiwa maji ya moto na mumewe baada ya kuchuma mahindi mawili (2) shambani bila ya ruhusa yake. Mumewe huyo alitoweka na ndugu za Neema walihofia kumchukua kwa kuogopa kudaiwa mahali iliyolipwa na mumewe kama taratibu za kumuoa.

“Hakuna ndugu yangu hata mmoja aliyejitokeza kunisaidia kipindi chote cha matibabu. Walihofia kama ningefariki ingempasa huyo ndugu kurudisha mahali ambayo mume wangu alitoa. Nilikuwa nasaidiwa na majirani tu, nilikata tamaa ya kuishi nilikuwa nasubiri siku yangu ya kufariki ifike,” anasimulia Neema.

Aidha, Neema anawashukuru watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela wakiwemo manesi na madaktari kwa upendo na msaada mkubwa waliompatia toka siku wanampokea katika hospitali hiyo mpaka sasa ambapo anatarajia kurudi nyumbani.

“Nawashauri watanzania wasisikilize maneno ya watu wanaolalamika kwamba Muhimbili huduma sio nzuri, si kweli,kwa muda wote niliokaa hapa nimepatiwa huduma nzuri, tena kwa upendo na upole”

Akielezea maendeleo ya afya ya Neema, Mkurugenzi wa Upasuaji ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji Dkt. Ibrahimu Mkoma amesema kwamba, Neema alipokelewa hospitalini hapo tarehe 06/07/2015 akitokea Mkoa wa Mara wilaya ya Musoma , Neema alikuwa na majeraha ya mwaka mmoja toka aunguzwe.

Mpaka sasa Neema ameshafanyiwa oparesheni tatu kwa nyakati tofauti, zilizohusisha kutengenisha baadhi ya viungo kwani shingo, kifua na mkono wa kushoto vilishikana. Halkadhalika ilibidi kutoa ngozi ya sehemu ya mwili ili kufunika sehemu zile zilizoathirika zaidi.

“Ni katika kipindi hicho cha matibabu, Mhe. Rais alimuona Neema na kuguswa na hali yake, ambapo aliamua kumsaidia mpaka hivi sasa mnavyomuona. Neema sasa amepona na ataweza kuihudumia familia yake vizuri”,  aliongeza Dkt. Mkoma.

Akiongelea Moyo wa kujali wanyonge alionao Rais JPM, Dkt. Mkoma anasema kwamba Rais anaongoza kwa mfano, hivyo watanzania hawana budi kujifunza moyo huo wa kujali na kusaidia wahitaji wakati wote kwenye jamii.

Aidha, Dkt. Mkama ametoa wito kwa wadau na taasisi zinazohusika katika kutoa elimu kwa umma hususan madhara ya vitendo vya kikatili kutoa elimu hiyo kwa kuzingatia sehemu zenye ukubwa wa tatizo hilo ili kumaliza kabisa majanga ya aina hiyo.

Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE