March 9, 2017

MAHAKAMA YAKATAA MAOMBI YA BODI YA WADHAMINI CUF


 
NA Kulwa Mzee wa gazeti la Mtanzania


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imebadili uamuzi wake wa kusikiliza maombi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), bila kuwepo wajibu maombi badala yake itasikiliza pande zote mbili zikiwepo.


Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri aliondoa uamuzi wa kusikiliza maombi ya zuio la muda upande mmoja badala yake kaamuru maombi yasikilizwe wakiwepo wajibu maombi, Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma (CUF) na wenzao sita.


Hakimu Mashauri alitoa uamuzi huo baada ya wajibu maombi wakiwakilishwa na Wakili Mashaka Ngole kufika mahakamani kuomba wapewe muda wa kujibu maombi.


Wakili Ngole alidai maombi hayana uharaka wowote kwani hakuna kinachoooza na uharaka huo haupo hivyo wapewe muda wajibu maombi kisha wasilizwe pande zote mbili.


Wakili wa waombaji, Hashimu Mziray alipinga kwa madai kwamba mahakama ilishakubali kusikiliza maombi upande mmoja hivyo kama anapingana na uamuzi huo akate rufaa, akitoa uamuzi huo Hakimu Mashauri alisema kwa hali halisi ya kesi, ili haki itendeke bila kucheleweshwa mahakama inaondoa amri iliyotoa ya kusikiliza maombi upande mmoja. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu.


Wakili Mziray aliwasilisha maombi madogo chini ya hati ya dharura, wakiomba mahakama iwazuie kwa muda wajibu maombi kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE