March 11, 2017

LAANA YA MTENGA NA WANA CCM IRINGA YAMTUMBUA MSAMBATAVANGU

jesca Msambatavangu akiteta jambo na aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga 
Na MatukiodaimaBlog 
Hakuna laana mbaya kama usaliti na iwapo aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu angemsikiliza aliyekuwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kabla ya kuhamishiwa mkoani Pwani kutokana na chuki za Jesca leo asingetumbuliwa ugenini 

Msambatavangu ni jina lililopata umaarufu sana mkoa wa Iringa na hivyo kutokana naumaarufu alijiona yupo juu ya kila mmoja kwa kutaka kumuona yupo chini yake, ifahamike suala hili lililomkuta leo Mtenga aliliona siku nyingi na hata kupaza sauti kuwa mwenyekiti ni msaliti 


Kwani hata Jimbo la Iringa mjini lilichukuliwa na chadema Kwa usaliti ambao leo chama kimeamua kumlipa ujira wake kwa kumtumbua bila ganzi kwa kumfukuza uanachama 

Mkoani Iringa hata viongozi mbali mbali na watu kadha wamevunjiwa heshima na Msambatavangu akiwemo Micheal Mlowe pia binafsi nilitumiwa ujumbe mzito wa vitisho na mwenyekiti huyu ambae leo ametumbuliwa. 

Mara zote alitumia nafasi yake vibaya kwa kutisha watu na hata wengine kushindwa kumweleza kuwa anakiua chama na leo kabla ya kikiua chama amekufa yeye kisiasa ndani ya CCM hii ni wazi chama hakijataka kufuga ugonjwa. 

Zipo taarifa kupitia wapambe wake ambao wamekuwa wakijigamba eti anahamia Chadema na Lowasa msaliti mwenzake atakuja kumpokea amini ni haki yake kwenda chama chochote ila itambulike kuwa CCM si chama cha kispoti spoti ni chama imara

Pia kupitia wapambe hao wamejipanga kufanya matukio ya vurugu mjini Iringa na kuwahamasisha wapambe wake kufanya maandamano eti kupinga kufukuzwa kwake 

Sina shaka hata kidogo na utendaji kazi wa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa mkuu wa mkoa Amina Masenza chini ya ulinzi imara wa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa RPC Julius Mjengi wapo kuona mkoa wa Iringa unakuwa shwari 

CCM no chama cha wana chama waaminifu na si chama cha wasaliti hivyo wana CCM Iringa wanasema nenda salama Jesca Msambatavangu ukawasaliti wazoefu wa kusalitiana Chadema sio ulichokuwa ukifanya kuvaa ngozi ya kondoo kumbwe umbwa mwitu mchana CCM usiku chadema 

Ungemsikiliza katibu wako Mtenga leo usingeaibika ugenini kweli sikio la kufa ni la kufa dawa haisaidii Kwa kuwa hukusikia la mkuu umelipata rungu la Mwenyekiti wa CCM Taifa John Pombe Magufuli 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE