March 19, 2017

KUWA NA WATOTO NA KUFANYA MAZOEZI KUNASAIDIA KUISHI MIAKA MINGI ZAIDI KULIKO WASIO NA WATOTO...... Manufaa ya kuwa na watoto huonekana hata wakati watu wanapotimia umri wa miaka 80 na zaidi.

Kuwa na watoto inaweza kuchangia mtu kuishi miaka mingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa.

    Watu wasiofanya mazoezi huzeeka haraka

Wataalamu kutoka kwa taasisi ya Karoliska mjini Stockhom nchini Sweden, walifuatilia maisha ya mtu kutoka umri wa miaka 60 kwa wanaume wote (704,481), na wanawake (725,290) waliozaliwa kati ya mwaka 1911 na 1925 wanaoishi nchini Sweden.

Waligundua kuwa wanaume na wanawake ambao walikuwa na takriban mtoto mmoja, walikumbwa na vifo vichache kuliko wanaume na wanawake wasio na watoto.
Image caption Utafiti wa awali ulionyesha kuwa watoto wasichana ndio wanaweza kuwasaidia wazazi wao uzeeni kuliko hata watoto wavulana.

Katika umri wa miaka 60, tofauti ya
Miaka ya kuishi kati ya wale walio na watoto na wasio nao, ni karibu miaka miwili kwa wanaume na mwaka mmoja unusu kwa wanawake.

Wakifika umri wa miaka 60, wanaume walio na watoto hutarajia kuishi miaka mingine 20.2 huku wanaume wasio na watoto wakitarajia kuishi miaka 18.4 zaidi ambayo ni tofauti ya mwaka moja unusu.

    Miaka 115 ndio 'mwisho wa maisha' kwa binadamu

Nao wanawake walio na umri wa miaka 60 walio na watoto hutarajia kuishi miaka 24.6 zaidi, huku wale wasio na watoto wakitarajia kuishi miaka 23.1 zaidi, ambayo ni tofauti ya mwaka moja unusu.
Haki miliki ya picha IYMEN BAERLI
Image caption Wazazi walio na watoto huishi maisha ya afya zaidi kuliko wale wasio na watoto.

Utafiti wa awali ulionyesha kuwa watoto wasichana ndio wanaweza kuwasaidia wazazi wao uzeeni kuliko hata watoto wavulana.

Nao uatafiti mpya unaonyesha kuwa wavulana wanaweza kuwasaidia wazazi sawa na wasichana ikiwemo kuwasaidia kupata matibabu.

    Utafiti: Chunusi humfanya mtu kuonekana mdogo

Hata hivyo watu wasio na watoto hupata wakati mgumu zaidi kupata huduma ambazo zinastahili kutolewa na watoto.

Sababu zingine ni kuwa wazazi huishi maisha ya afya zaidi kuliko wale wasio na watoto.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE