March 20, 2017

KATIBU WA CCM WILAYA YA MUFINDI AJITOSA KUCHUKUA FOMU UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

Jimson mhagama kulia akimwelekeza jambo aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba, Mhagama ni mmoja kati ya wana CCM waliochukua fomu kuwania ubunge Afrika mashariki 
Mhagama akiwa katika mkutano wa kampeni za udiwani, ubunge na Urais mwaka 2015 wilaya ya Mufindi ilifanya vema katika uchaguzi huo
Mhagama kushoto akiwa na mzee wa matukiodaima 
.............................................
Na MatukiodaimaBlog
Zoezi la uchukuaji fomu za kuomba kuchaguliwa kuwa mbunge wa Afrika Mashariki umeendelea huku kada maarufu wa CCM aliyetabiriwa kufika mbali na aliyekuwa mwenyekiti wa Taifa wa ccm Jakaya Kikwete, Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Jimson Mhagama kujitosa nafasi hiyo. 

Jimsoni Mhagama ambae ni kijana mdogo na mchapa kazi ambae katika wilaya yake ya Mufindi alipambana na kuusambaratisha upinzani katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 amesema ana uwezo mkubwa kuwatumikia watanzania kwa nafasi hiyo. 

Kwani amesema uwezo na nia anayo na elimu yake imamtosha kuwajibika kwenye nafasi hiyo. 

Alisema ana elimu ya Masters of Business Administration ( Degree mbili) hivyo hatashindwa kuwatumikia watanzania na Afrika mashariki kama ninhem. 

safari ya Mhagama kwenye nafasi hiyo ni moja kati ya utekelezaji wa maono ya viongozi mbali mbali kama aliyekuwa mwenyekiti taifa wa CCM Jakaya kikwete na aliyekuwa katibu mkuu CCM  Yusuph Makamba ambao wakiwa ziarani mkoani Iringa kwa nyakati tofauti walisifu uongozi wake kama katibu mkuu msaidizi wa CCM mkoa wa Iringa. 


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE