March 19, 2017

INJINI MPYA YA KURUSHA ROKETI YAFANYIWA MAJARIBIO KOREA KASKAZINI....

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anasemekana ametaja uzinduzi huo kama wa "kihistoria"

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, vinasema kuwa taifa hilo limefanyia majaribio injini moja kubwa maalum yenye uwezo wa kurusha angani mtambo wa Satellite.

Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, amenukuliwa akisema kuwa, injini hiyo mpya itaisaidia Korea Kaskazini, kufikia uwezo wa kimataifa wa kufyatuaji Satellite angani.

Wachanganuzi wanasema majaribio ya mtambo huo wa kurusha angani roketi--ambayo bado haijathibitishwa-- pia itakuwa jambo la kuangaliwa kwa undani katika nia ya Pyongyang kuunda zana za kinuklia zenye masafa marefu.

    China yaionya Marekani kuwa makini na Korea Kaskazini

    Je dunia itaifanya nini Korea Kaskazini?
    China: Marekani itatue mgogoro wake na Korea Kaskazini
    Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini

Tangazo hilo linatokea wakati wa waziri wa maswala ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, anapofanya mazungumzo na viongozi wa China huko, Beijing.

Awali, Bwana Tillerson, aliionya Marekani kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, kwamba inaweza kuharibu mambo hata zaidi.(habari na BBC)

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE