March 9, 2017

DIWANI WA CHADEMA ASIMAMISHWA KWA KUSHINDWA KUSOMA

Mh.diwani Julist Kisoma
............................................


Na MatukiodaimaBlog Mufindi

DIWANI wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Boma katika Halmashauri ya mji Mafinga  Julist Kisoma anayedaiwa kutojuakusoma na kuandika azua taflani kikaaoni kwa kugoma kusomataarifa za shughuli za kimaendeleokatika kata yake na kupelekea kusimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vyabaraza la madiwani .

Hatu ya diwani huyo kusimamishwa ilimkumba jana (machi 8) wakati wa kikao cha kawaida cha kila diwani wa kata kuwasilisha taarifa yashughuli za kimaendeleo kwenye kata yake na diwani huyo nafasi yake yakusimamia kuwasilisha taarifa ilikuwa yatisa baada ya kufika zamu yake kusoma taarifa hiyo kwa madai kuwa wakati ikiandaliwahakuwepo .

Diwanihuyo alikataa kusoma taarifa hiyo na kuibua mvutano mkubwa uliodumu kwa muda wa dakika kama 40 hivi pasipo kufikia muafaka huku akijitetea .

Kabla ya kufikia maamuzi ya kumpa adhabu diwani huyomadiwani waliomba Mwongozo kwa Mwenyeiti wa Halmashauri nakumtaka Mwanasheria wa Halmashauri hiyo kusoma kanuni na sheri zinavyosema endapo diwaniatakataa kusoma taarifa kwa makusudi na kudharau kiti atatolewa nje ilikujadiliwa na iwapo ataendelea kudharau atachukulia hatua za kinidhamu .

Mwenyekitiwa Halmashauri ya mji wa Mafinga Charles Makoga alisema kuwa kanuni ya 18[1] katika mkutano wowote wa Halmashauri kama mjumbe ataonyesha kukosaheshima kwa madaraka aliyonayo mwenyekiti ana kudharau kanuni za Halmashaurikwa kuzuia kwa makusudi shughuli za Halmashauri zisiendelee au vinginevyo kuwamwenyekiti ataelekeza mkutano kwatukio hilo kwa kumtaja jina mara tatu mtu anaeyehusikana.

“ ….iwapomjumbe ataendelea kudharau madaraka ya mwenyekiti basi mwenyekitataliombabaraza kuairisha shughuli za mkutano na kutafakari jambo hilo…baada ya kukaa nakutafakari jambo hili..diwani Julius kisoma anakosa la kutoheshimu kiti kukaidikusoma taarifa na kwenda kukaa bila kuamliwa na Mwenyekiti..hivyo basi kwamamlaka niliyopewa kutokana na dharau hii ninamsimamisha kutohudhuria vikao vitatu vya baraza na kamati za madiwani nakupoteza haki zake za msingi alizokuwa akizipata kipindi hicho..pia naiagizakamati ya maadili ndani ya mwezi mmoja wakae na kujadili na kuleta taarifasahihi katika kikao kijacho” 

Alisemakwa mara nne mfululizo diwani huyo amekuwa akikataa kusoma taarifa na mara nyingine akijitetea kuwa ana tatizo la kutoona vizurina wakati mwingine akiomba kusaidiwa kusoma taarifa ya kata yake .

Akizungumzabaada ya adhabu hiyo Kisoma alisema kuwa ameshindwa kusoma taarifa hiyokutokana na kutoshiriki vikao vya kata vilivyoiandaa taarifa hiyo hivyohakupenda kusoma taarifa ambayohakuiandaa kuwa tarifa hiyo iliandaliwana afisa mtendaji wa Kata na kamati yake hivyo hawezi kusoma na kuwasilishakitu asichokijua.

Diwani huyo hii ni mara ya pili kukutwa na adhabu katika baraza hilo kwa mara ya kwanza alisimamishwa na kutokana na kutojua kusoma na kupelekea chama chake kanda ya Nyasa kupinga uamuzi huo na kuwa diwani wao anajua kusoma na kuandika kabla ya safari hii kugoma kusoma taarifa kwa sababu zinazofanana na zile za awali
Kwa mujibu wa taratibu mwenyekiti wa halmashauri hana mamlaka ya kumsimamisha ama kumuwajibisha diwani yeyote Kwa kutojua kusoma ama kuandika iwapo alidanganya wakati wa kujaza fomu mwenye mamlaka ya kuchukua hatua ni tume ya uchaguzi baada ya mwenyekiti wa halmashauri kumwandikia barua ya taarifa mkuu wa mkoa ili aunde tume kuchunguza na kuijulisha tume baada ya uchunguzi na si vinginevyo 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE