March 31, 2017

DC TUNDURU AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI MRUSHA NA SEMENI`


```Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera ameanza ziara ya kufuatilia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi ya shule za msingi, katika ziara hio Mhe. Homera aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Tunduru Bw. Chiza Marando.```

```Ziara hio ilianzia shule ya Msingi Semeni iliyopo kata ya Mtina ambapo Mkuu wa wilaya alikutana na kamati ya ujenzi wa shule hio, Mwenyekiti wa kamati hio Bw. Hamidu Saidi alimueleza Mkuu wa wilaya kuwa wamepokea shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa darasa moja na wapo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi.```

```"Mkuu wa wilaya mbele yako ni kamati ya ujenzi ya shule ya msingi semeni na tunakiri kupokea shilingi milioni kumi ambayo tunatarajia kujenga darasa moja".```

```DC Homera aliagiza ujenzi uanze mara moja kwa kuwa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ilitoa fedha toka mwaka jana lakini cha kushangaza hadi sasa ujenzi haujaanza, alieleza kuna tatizo kwenye uongozi wa kijiji na alitoa agizo ujenzi uanze ndani ya siku sita.```

 ```"Naagiza ndani ya siku sita mchanga uwe umefika ili ujenzi uanze mara moja, na Mwenyekiti wa kijiji hiki cha semeni Bw. Yusuf Kanduru Mpelembe namuagiza aje ofisini kwangu kwa kuwa nimepata taarifa zake za kuendekeza migogoro kijijini na shilingi milioni kumi mliopewa na Halmashauri ya wilaya ya Tunduru inatosha kujenga vyumba viwili vya  madarasa na ofisi moja kwa kuwa kijiji kina benki tofali hii itasaidia kupunguza garama".```

```Aidha akiwa shule ya msingi Mrusha iliyopo kata ya Mchesi Tarafa ya Lukumbule alikagua ukarabati wa sakafu ya madarasa mawili na kuagiza darasa lililobomoka ukuta lianze kujengwa upya.```

```"Nakuagiza Mwalimu Mkuu ndani ya wiki mbili sakafu ya vyumba viwili vya madarasa ukarabati ukamilike na hela itakayo bakia uanze ujenzi wa msingi wa darasa jipya".```

```Mkuu wa wilaya alimalizia kwa kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mrusha kwa kuwapa motisha na kuwa sisitizia umuhimu wa elimu ili waweze kufanikiwa hapo baadae na aliwachangia shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kununua sukari ya uji ambayo wanafunzi hao hunywa saa nne muda wa mapumziko.```

```Kwa upande wake Dc Homera alifurahishwa na hatua ya shule ya msingi Mrusha kuvuka lengo la agizo lake la kila shule kupanda hekari tano za miche ya mikorosho, shule hio imepanda hekari nane.```

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE