March 25, 2017

DC LUDEWA TSERE AKAMATA MTUHUMIWA ALIYELIMA BANGI KWA MADAI NI KINGA YA MIFUGO YAKE ISIROGWE NA WACHAWI .........

Mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsere  (kushoto)  akimsimamia mtuhumiwa  wa bangi kuteketeza bangi  hiyo  ambayo anadai alilima kwa  ajili ya  kinga   ya ng'ombe kutorogwa na wachawi

Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa Andrea Tsere akiwa katika msako  wa bangi kwenye  misitu ya  kijiji  cha Kitewele  ambako alifanikiwa  kuteketeza  shamba ekari  moja la bangi


Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa Andrea Tsere kushoto akiwa na kamati ya  ulinzi na usalama wilaya hiyo wakishiriki  kufyeka kwa  lengo la  kuteketeza  shamba la bangi  kijiji  cha Kitewele 
............................................................................................................................................................
MKUU  wa  wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe  Andrea Tsere ameendesha  msako  wa mapambano  dhidi ya  dawa  za  kulevya  wilayani   humo kwa kukamata shamba la bangi  ambalo mtuhumiwa anadai  alilima kwa  ajili ya dawa ya  kuzuia mifugo yake kinga  na wachawi 

Mkuu  huyo wa  wilaya  ambae ni mwenyekiti wa kamati ya  usalama  wilaya ya Ludewa kwa kushirikiana na kamati yake ya usalama walifanya msako  huo jana  kwa  kukamata na kuliteketeza shamba lenye ukubwa wa  ekari moja katika kijiji cha Kitewele kata ya Mawengi wilayani hapa Mwandishi wa mtandao huu wa matukiodaimaBlog ,Maiko Luoga anaripoti  kuwa .

Shamba hilo  la bangi  linadaiwa kuwa ni mali  kijana  Ebelehadi Haule mkazi wa kijiji na kata ya Mawengi wilayani Ludewa  na tayari amekiri kumiliki shamba  hilo lililokuwa katika  eneo la msitu mkubwa uliopo katika kijiji cha Kitewele akidai kuwa anaitumia kulisha mifugo yake kama dawa ili isirogwe na wachawi.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Madunda   Peter Ng,ingo alisema kuwa kuwa kabla ya kumjulisha mkuu wa  wilaya juu ya uwepo  wa shamba hilo  la bangi alipata taarifa toka kwa  wasamalia wema wakazi wa  kijiji cha Madunda ndipo yeye kama Mtendaji akafikisha taarifa katika mamlaka husika pamoja na kumkamata muhusika aliyelima bangi hiyo.

Akizungumza akiwa katika eneo la tukio mkuu  wa wilaya ya Ludewa  Tsere mbali ya  kuonya wananchi  kuachana na kilimo  cha bangi na matumizi  mengine ya  dawa  za  kulevya bado aliwashukuru wananchi kwa  kutoa taarifa  za uharifu  huo na kuwataka kuendelea  kutoa taarifa ya watu ama mtu anayejihusisha na kilimo  cha  bangi na uharifu mwingine 

Tayari  jeshi la polisi mkoa wa  wilaya na mkoa wa Njombe limeendelea na mapambano  dhidi ya dawa za  kulevya  na hivi karibuni  mkuu wa mkoa wa Njombe  Christopher Ole  Sendeka alifanya msako kama   huo  wilaya ya Makete na kuteketeza mashamba ya bangi .

IWAPO  WEWE  NI MKUU  WA  WILAYA AMA UNATAARIFA  YA  UWEPO  WA KILIMO  CHA BANGI SEHEMU  YEYOTE NCHINI  TUMA  TAARIFA  YAKO KWA WHTASAP - 0754 026299

KWA  PAMOJA TUUNGANE NA  RAIS  WETU  KUIFANYA  TANZANIA  SALAMA BILA DAWA  ZA  KULEVYA  Image result

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE