March 11, 2017

DC KASESELA AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA INSTAGRAM PHOTOGENIC

MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amekabidhi zawadi mbali mbali kwa washiriki wa
Mashindano ya Instagram photogenic competition yamefikia kilele hivi karibuni

Tukio la kukabidhi zawadi hizo limefanyika jana baada ya mkuu wa wilaya kutoka katika mapumziko ya mkutano mkuu SAGCOT uliokuwa ukifanyika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam


David Mtengile maarufu kwa jina la
C.E.O Dmplanet ambae ni mratibu wa mashindano hayo alisema kuwa  zawadi hizo zimetolewa kwa baadhi wa washindi wa top five waliokuwa wamesalia kutoka mkoa wa Dar es Salaam.

Kuwa Shindano hilo linaendeshwa katika mtandao wa instagram kwenye page inayoitwa @dmplanet_tz na kuwa
mashindano zaidi yataendelea kufanyika lengo ni kuhamasisha matumizi sahihi na yenye fursa kupitia mitandao ya kijamii.

Alisema kwa kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wadau kushiriki mashindano hayo na kuwa jumla ya washiriki wote walikuwa 135 kutoka kila kona ya Tanzania.

Na kuongeza kuwa mzunguko wa kuchuja ulifanyika mpaka kufikia tano bora  na ndipo mshindi alipopatikana wa kwanza hadi wa tano kutokana na likes wakizopaata.

Mratibu huyo alisema nafasi ya kwanza ilishikwa na mwanadada kutoka Iringa anayeitwa Emida Elmerik
akifuatiwa na Ana mbawala (Dar es salaam)
tatu ikishikwa na Khizer (Dar es laam)
.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE