March 5, 2017

CRDB IRINGA YAWAFUNGUA WANAWAKE

Meneja  wa  CRDB Iringa  Kissa  Samweli akielezea  lengo la  warsha  ya   wanawake mkoa wa Iringa  kuelekea  siku ya wanawake  duniani inayofanyika kila mwaka machi nane mbele ya viongozi  mbali mbali jana  , kutoka  kushoto ni katibu  tawala wa  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayubu , mkuu wa mkoa wa Iringa  Amina Masenza na wa kwanza  kulia ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela
Washiriki wa  warsha hiyo  wakifuatilia  kwa makini  ufunguzi
Katibu tawala  wa  mkoa wa Iringa  Wamoja  Ayubu  akizungumza na washiriki  wa  warsha  hiyo  ya  wanawake iliyoandaliwa na benki ya CRDB Iringa , kulia kwake ni  mkuu wa  mkoa  Amina Masenza , meneja wa RCDB Iringa Kissa Samweli na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  wakifuatilia
Mkuu wa wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  akimkaribisha  mkuu wa  mkoa  kufungua warsha hiyo
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akifungua  warsha ya  siku moja ya  wanawake Iringa  iliyoandaliwa na benki ya  CRDB kuelekea siku ya  wanawake duniani Machi 8
Baadhi ya  washiriki wakiwa katika warsha hiyo
Afisa biashara  wa CRDB Iringa Sophia Nyoni akitoa mafunzo ya biashara
Veronica  Kaundama akifuatilia mafunzo hayo
Wataalam  kutoka  CRDB Iringa
RC  Masenza  akiwaasa wanawake  kutokubali  waume zao kuwekea hati za  nyumba dhamana  bila  kushirikishwa
Mwezeshaji kutoka CRDB Iringa  akiwapa  elimu ya  kiuchumi  washiriki  wa  warsha hiyo
Na MatukiodaimaBLOG 

WAKATI   Machi 8  ni  siku   ya  wanawake  dunianibenki  ya  CRDB  tawi la  Iringa  imewataka  na  wanawake  mkoani  Iringa  kwa lengo la  kupokea  changamoto mbali mbali  za kiuchumi  zinazowakabili  hadi kupelekea baadhi ya  wanawake   kukopa pesa  za  riba  kubwa .

Meneja  wa CRDB  mkoa  wa  Iringa  Kissa  Samwel  akimkaribisha  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza   kufungua  warsha ya  siku moja ya wanawake mkoani hapa  iliyofanyika mjini  Iringa ,jana  alisema kuwa   lengo la   warsha   hiyo  ni  kuwawezesha  wanawake hao  kutoa  changamoto   zao zinazokwamisha  kusonga  mbele  na  wao kama  taasisi ya  kifedha  kuangalia  namna ya  kuwashauri  njia  sahihi  za  kupita .

Alisema  kuwa   wao kama CRDB  wameona ni  vema  kukutana na  wanawake hao  kama  sehemu ya  kuadhimisha  wiki  ya  wanawake duniani  na kuwa  sababu kubwa  ambayo  wanaiona ni  kikwazo kwa  wanawake  kunufaika na  fursa mbali mbali ni baadhi yao  kutofikiwa na  elimu  sahihi  za  njia ya  kuweza  kufika katika taasisi za  kifedha  kukopa .

Meneja  huyo  alisema  kuwa chini  ya  kauli mbinu Tanzania ya  viwanda  wanawake Msingi  ni msingi wa mabadiliko kiuchumi  kwa  upande wa  benki  yake  kuna mikopo  mbali mbali inatolewa na marejesho  yake  yanautaratibu mzuri  zaidi  ambao  kila mmoja anaweza  kuumudu  kuliko  mikopo  wanayoendelea  kukopeshwa  mitaani na  watu  wanaotafuta  kujinufaisha  kwa  kuwatoza  riba  kubwa na hata  baadhi yao  kujikuta  wanauziwa mali  zao kama  nyumba   na mali nyingine .

kizungumza na  anawake hao  mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina  Masenza  alivitaka  vyombo  vyote  vinavyohusika  na  sheria pasipo  yeye  kuingilia muhimili   aliviomba  kusaidia  mwanamke  ambae analazimika   kunyanyasika  katika  familia kwa kukopeshwa  pesa za  riba  kubwa na baadhi ya  wanaume wanaukopea mikopo  nyumba ama mali za familia pasipo   mwanamke  kuhusishwa .

“ Kipekee  niwaombe  wanawake  kupeni  benki  chombo  ambacho  hakipo kwa  ajili ya  kutapeli  mali yako ama  kukunyanyasa kama  wakopeshaji wa mitaani ……na mkopo  ambao utakopeshwa benki  utakuwa  umepewa  elimu  ya  namna ya  kuutumia na  kuurejesha ….ila  kwa upande wa mahakama mwanaume  anakuja  na hati ya  nyumba kwa  ajili ya kuiwekea  dhamana huku baadhi yao  wakidanganya kufoji picha na  sahihi ya  mke  na ninyi mkiamini  kuwa  huyo  mwanamke  aliyeweka  sahihi na  picha ni mke  wake  wa  ndoa tunajifunza  kuwa wanaume  wengi  hudanganya kwa  kwenda na  vimada benki ya mahakamani kuapa  ili  kupata  mikopo na baadae wake  halali  huishia  kupoteza mali  ….katika  hili  naomba sana mahakama  tusaidiane   kuona  wanawake  hawapotezi mali zao “

Hivyo alishauri  idara ya  mahakama  kuangalia  njia  nyingine ya  kuwabana  wanaokwenda  kusaini hati  za  mikopo  kama kweli  walioweka  sahihi ni  wake zao halali ama  lah.

Mkuu   huyo wa  mkoa  alisema kuanzia sasa  wanawake  wote wa  mkoa wa Iringa  wanaagizwa kutunza hati  mbali mbali za mali  zao Pamoja na  vyeti  vyao  vya taluma  ili kuepuka kulizwa na  baadhi ya  wanaume   wasio na nia njema ya  kuitazama  familia .
MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE