March 18, 2017

BREAKINGNEWS RC IRINGA ANUSURIKA KIFO GARI LAJERUHI WAWILI WAKIWA KATIKA MAZOEZI

Askari polisi wakiwa wamemkamata dereva taxi aliyesababisha ajali
Askari magereza akiwa chini baada ya  kugongwa  na gari  asubuhi hui wakiwa katika mazoezi
watu wawili wamenusurika kifo baada ya gari dogo aina ya taxi kuwagonga wananchi waliokuwa katika mazoezi asubuhi ya Leo mjini Iringa huku mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akinusurika

Ajali hiyo imetokea nje ya lango la kamanda wa polisi mkoa dakika tatu baada ya kuanza mazoezi kuelekea uwanja wa samora 

Hata hivyo katika ajali hiyo iliyosababishwa na uzembe wa dereva aliyekaidi amri ya askari wa usalama barabarani ambao walisimamisha gari hilo lililokuwa likitoka mwelekeo mmoja na wafanya mazoezi hao

Majeruhi hao wamepata michubuko kiasi mwilini huku mkuu wa mkoa ambae alikuwa karibu na majeruhi huyo hakuguswa kabisa na gari hilo japo alikuwa karibu na majeruhi hao 

Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa

Habari kamili itakujia hivi punde tunaomba radhi kwa picha zisizo kuwa na ubora

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE