March 9, 2017

BARCELONA WAMEUSHANGAZA ULIMWENGU TENA USIKU WA KUAMKIA LEO

Unaweza usiamini lakini ni kawaida kutokea katika mchezo wa soka, inawezekana leo asilimia kubwa ya watu waliyotabiri mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya FC Barcelona dhidi ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ungemalizika kwa PSG kutolewa.

Barcelona aliingia katika mchezo huo akiwa tayari yupo nyuma kwa goli 4-0 alizofungwa na PSG katika mchezo wa kwanza, hivyo kwa sheria za mpira Barcelona alikuwa na nafasi pia licha ya kuwa kwa uhalisia inawezekana Barcelona wengi walikuwa wanaangalia game hiyo wakiamini kuwa wanakamilisha ratiba tu.

Mambo yamekuwa tofauti na FC Barcelona wameushangaza ulimwengu wa soka kwa kuifunga PSG goli 6-1 katika mchezo wa marudiano uliyochezwa Nou Camp, ushindi huo wa FC Barcelona unaiondoa PSG kwa kuifunga jumla ya goli 6-5 hiyo ni baada ya kujumlisha magoli ya michezo yote miwili.

Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Luis Suarez dakika ya 3, Kurzawa wa PSG alijifunga dakika ya 40, Lionel Messi aliyefungwa kwa penati dakika ya 50, Neymar aliyefunga mawili dakika ya 88 na 90 kwa penati la mwisho alifunga Sergi Roberto dakika za nyongeza Ednson Cavani ndio alifunga goli la kufutia machozi kwa PSG dakika ya 90.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE