March 15, 2017

BAADA YA VIROBA KUPIGWA MARUFUKU , BIASHARA YA ULANZI YAPATA UMAARUFU MKUBWA IRINGA

Gari  lililobeba  pombe  aina ya Ulanzi  kutoka  Iringa  vijijini  likipeleka pombe  hiyo  kuuzwa mjini Iringa  ,pombe  ambayo  imechukua nafasi ya  viroba  kutokana na kuuzwa kwa  bei ya chini kwa  lita
Usafirishaji wa  Ulanzi  wawaingizia kipato  wananchi Iringa


HUKU jeshi   jeshi  la  Polisi mkoa wa Iringa  likiendelea na msako   huo dhidi ya  biashara ya  viroba  baadhi ya  wafanyabiashara  wa  vivywaji mkoani hapa   wameomba  serikali kulitafakari  upya  suala  hilo kwani linayumbisha  uchumi  wao kutokana na baadhi yao  kununua vinywaji  hivyo kwa  pesa   mikopo   hivyo kuzuia ni kuwafanya wapoteze  pesa  walizotumia na kulazimika kuingia katika deni juu ya  deni .

Wakizungumza mtandao huu wa matukiodaimaBlog pasipo  kutaja majina  yao  wafanyabiashara wa  eneo la vibanda vya  CCM mjini Iringa  walisema  kuwa kuzuiwa kwa  viroba kumeyumbisha biashara   zao  kwa maana ya hofu ya  kupata  pesa za   kulipa madeni waliyokopa kwa  ajili ya  kununulia viroba na  pili   wamepoteza wateja wengi ambao  walikuwa  wakifika kunywa  pombe   hiyo ya  viroba .

" Zamani tulikuwa  tunauza hadi kufikisha 200,000 kwa  siku  kwa sisi  wafanyabiashara  wa grosari ila  toka  wamezuia  viroba  biashara  imeshuka wakati  mwingine hadi unafika muda wa  kufunga mauzo  ni chini ya 50,000 na hapo  hapo  unadaiwa  kodi ya  pango ,vicoba  na pesa  ya matumizi yaani tumeyumba  kweli "

Waliiomba  serikali  kuruhusu wafanyabiashara  hao  kuendelea  kuuza pombe   hiyo ya  viroba kwa  kupima kwenye chombo maalum na  wanywaji  kutumia grasi badala ya kuendelea  kutumia viroba hivy  ambavyo  vinachangia  uchafuzi wa mazingira .

Kuwa   hivi  sasa   maeneo  wanayouza  zaidi ni  yale  ambayo  wamechanganya bia na pombe  za kienyeji kama  ulanzi na  komoni ambazo  zinauzwa kwa bei ya  chini ila wale  wanaoendelea  kuuza bei  pekee yake wateja  wamewakimbia .

Hata  hivyo  uchunguzi wa mtandao wa matukiodaimaBlog umebaini  kuwa biashara  hiyo ya  viroba kwa  sasa  mjini Iringa na  vijijini imekuwa  ikiuzwa kwa siri  kubwa na wengi  wanatumia majina mapya  badala ya  kuita viroba wanapohitaji pombe  hiyo wanaitaja kwa  jina la  marufuku  moja na wengi  wao  wamelazimika  kuhifadhi  pombe   hiyo kwenye ndoo kwa  kuchanganya na pombe ya ulanzi  .0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE