March 6, 2017

AJALI BASI LA ABOOD KUGONGA MAGARI 2 YAJERUHI 11 KITONGA IRINGA


WATU  11   wamejeruhiwa katika  ajali ya basi la kampuni ya Abood lenye  namba za  usajili  T229 AZG baada ya  kuyagonga hadi  kupinduka magari mawili  likiwemo  lori lililobeba  ndizi  kutoka Mbeya  kwenda  Dar  es Salaam lenye namba  za usajili  T 191 CXU na basi la kampuni ya Happy National lenye namba  za usajili T 427 DDT yote  yakitokea  Mbeya  kwenda Dar es Salaam .


Ajali  hiyo  imetokea  jana majira ya saa 8  mchana  katika eneo la Mlima kitonga wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa kwenye  barabara ya  Iringa - Dar es salaam .


Majeruhi wa ajali  hiyo  walimweleza mwandishi  wa mtandao wa matukiodaimaBlog  kuwa chanzo cha ajali  hiyo  ni basi la Abood  kufeli  breki na  hivyo  kuyagonga magari zaidi ya matatu  huku  mawili yakitumbukizwa  bondeni na  mengine  yakikwaruzwa ubavuni .


Sarah   Emmanuel ni mmoja kati ya majeruhi aliyekuwepo katika  basi hilo la Abood  alisema kuwa baada ya basi hilo kufeli  breki  dereva  aliwataka  abiria  wote  kurudi nyuma ya asi hilo kwa ajili ya usalama  wao  kutokana na basi kukosa  mwelekeo .


" Kweli  tunampongeza  dereva   wetu  hakuonyesha  kukata  taamaa alijaribu   kwa  uwezo  wake wote  kuokoa maisha  yetu  na vinginevyo tungepoteza maisha  wote ......kweli mbali ya  kujeruhiwa  ila siwezi kumulaumu  dereva  kwa ajali  hii nampongeza sana  alikubali  kufa pekee yake  kuokoa roho zetu "

Mbunge  wa  jimbo la  Kilolo  Venance  Mwamoto akizungumza eneo la  tukio alisema  kuwa baada ya  kupata  taarifa ya  ajali  hiyo  akiwa katika  ziara  yake ya  kukagua ujenzi wa barabara  ya  lami  mji mdogo wa Ilula   eneo la soko la Tasaf  alilazimika  kukimbia  eneo la  tukio kwa ajili ya  kutoa msaada kwa gari lake  kutumia kama gari la  wagonjwa kutokana na  Hospitali  teule  ya  wilaya ya  Kilolo Ilula  kuwa na gari  moja  pekee la  wagongwa .


Hata  hivyo  mbunge  Mwamoto  alisema  kuwa jitihada  kubwa  zinafanywa na  dereva   huyo  kuokoa maisha ya  abiria  wake  kwani  angekuwa  dereva mwingne  mara  baada ya  breki  kufeli  basi angeruka na  kuacha abiria  wapoteze maisha .


Alisema  eneo hilo  ni  eneo lenye  kona  nyingi na mteremko mkali  ila bado dereva  aliweza  kulimudu  vema  basi hilo na kuwataka  madereva  kufanya  ucchunguzi wa breki  za  magari yao  pindi  wanapoanza mteremko  mkali wa Kitonga .


Mkuu wa mkoa  wa Iringa  Amina  Masenza  akitoa  pole kwa majeruhi  wa ajali  hiyo katika Hospitali ya  Ilula na Hospitali ya mkoa  wa Iringa  alisema kuwa serikali ya  mkoa  wa Iringa  kupitia kamali ya ulinzi na usalama na  ile ya usalama barabara  wanatarajia  kujenga  kituo  cha  polisi kidogo katika eneo la mlima  kitonga kwa  ajili ya kutazama usalama .


Pia  alimpongeza mwenyekiti wa kamati ya  usalama  barabarani Salim  Asas  kwa  jitihada  zake  mbali mbali ambazo  ameendelea  kujitolea kwa ajili ya kusaidia kamati  hiyo kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi na kila ajali inapotokea mwenyekiti  huyo  hufika  kutoa  msaada kwa majeruhi jambo ambalo ni kupongezwa na la baraba machoni pa Mungu .


Mkuu  mkoa  alisema  kuwa kati ya  watu  11  waliojeruhiwa sita kati  yao  wamelazwa  Hospitali ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa  akiwemo  dereva wa basi la Abood huku  majeruhi  watano  wapo Hospitali teule ya  wilaya ya  Kilolo  (Ilula  )  wakiendelea na matibabu .



0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE